KLABU ya Coastal Union imesajili wachezaji 13 ambao wataitumikia timu hiyo katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao Tanzania bara unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba mwaka huu hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa wachezaji ambao wamesajiliwa wametoka timu mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi. Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Abasalim Chidebele ambaye ni mshambuliaji kutoka timu ya Stand United, Kiungo Mkabaji Adeyum Salehe kutoka JKU ya Zanzibar, Kiungo Mshambuliaji Nasoro Kapama kutoka Ndanda FC ya Mtwara, Beki wa kati Ernest Mwalupani kutoka Ndanda FC ya Mtwara.
Wengine ni Beki wa Kushoto, Yassin Mustapa Salim kutoka Stand United, Kiungo Sultan Juma kutoka klabu ya African Sports, Mshambuliaji Ahmde Shiboli kutoka Klabu ya African Sports, Mohamed Hamis Mititi ambaye ni mchezaji huru.
Assenga amewataja wachezaji wengine kuwa ni Benedict Haule ambaye alisajiliwa akiwa kama mchezaji huru ambaye ni mlinda mlango,Mshambuliaji Ismail Mohamed Suma kutoka Stand United, winga wa kushoto ambaye ni mchezaji huyo Patrick Protas Kamuhagile.
Alisema wachezaji wengine ni Jackson Sabweto ambaye ni Mlinda Mlango kutoka Klabu ya VILLA FC ya nchini Uganda amesaini mkataba wa miaka miwili, Yossouph Sabo kutoka Klabu ya Younde FC ya Cameroon ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja. Wachezaji wa zamani waliobaki kutimukia klabu hiyo kuwa ni Bakari Mbwana “Kibacha”, Abdallah Mfuko, Hamadi Juma, Ibrahim Chuma, Ike Bright Obina, Abdulhalim Humud, Godfrey Wambura, Ayoub Semtawa na Sued Tumba.
Wakati huo huo wachezaji uongozi wa Coastal Union umewapandisha wachezaji watano kutoka timu ya vijana ya Coastal Union kutokana na uwezo wao kuwa mzuri na wa kuridhisha. Waliopandishwa ni Mohamed Shekuwe, Sabri Sabri, Tumaini Bakari, Fikirini Suleiman na Mtenje Albano