Mabingwa wa zamani wa Mpira wa Miguu Tanzania bara, Coastal Union ya Tanga imeondoka Tanga jana Alhamis kuelekea mkoani Shinyanga kucheza na timu ya Mwadui FC ambayo imepoteza michezo miwili kati ya mitatu iliyopita ya ligi kuu Tanzania bara.
“Wagosi wa Kaya’ waliifunga Yanga SC kwa magoli 2-0 katika mchezo wao wa kwanza wa mzunguko wa pili, kisha badae wakawachapa 1-0 Azam FC wiki iliyopita wanaamini wanaweza pia kuwafunga vijana wa kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ katika uwanja wao wa Mwadui Complex siku ya Jumamosi.
“Mashabiki wetu nawaomba waendelee kutuunga mkono, nawahakikishia upepo mbaya tayari umeshapita katika timu yetu hivyo tumejiandaa kwa mchezo ujao dhidi ya Mwadui FC naimani tutafanya vizuri.”