Meneja wa NSSF mkoani Dodoma, Kirondera Nyabuyenze akizungumza fursa mbalimbali zitokanazo na shirika la NSSF, Nyabuyenze amewataka watu mbalimbali wajitokeze kwa wingi kujiunga na NSSF, ili kujipatia fursa mbalimbali zikiwemo mikopo, matibabu na mambo mengiyo mbalimbali.
Mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM, akizungumzia fursa mbalimbali alizokumbana nazo na namna alivyozifanyia kati na kujipatia sehemu ya mafanikio katika kupambana na maisha. Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group, imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo Kigoma, Tabora, Singida, Mtwara, Mbeya, Iringa sambamba na ndani ya Dodoma, semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
Picha anuai juu ni sehemu ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo ya kamata fursa twendzetu, mkoani Dodoma.
Msanii mahiri wa Kughani Mashairi kwa mtindo wa kisasa kabisa, Mrisho mpoto akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake waliojitokeza mapema kwenye semina ya kamata Fursa twendzetu, iliofanyika ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya Africans dream, iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma. Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group, imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo Kigoma, Tabora, Singida, Mtwara, Mbeya, Iringa sambamba na ndani ya Dodoma, ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
Baadhi ya wasanii ambao wamenufaika mara baada ya kujiunga na Shirika la NSSF,shoto ni Queen Doreen na Mwasiti wakijadiliana jambo na mdau Phillipon mapema wakati semina ya Kamata fursa twendzetu ilipokuwa ikiendelea.