Na Andrew Chale
WADAU mbalimbali wa burudani usiku wa kuamkia jana walifurahia kwa pamoja na kula keki ya miaka 20 ya klabu ya Kimataifa ya Bilicanas na miaka 13, ya Clouds Fm, iliyoambatana na shamrashamra mbalimbali ndani na nje ya ukumbi huo.
Sherehe hizo ziliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bilicanas Group, Dk. Lilian Mtei ambapo aliwashukuru wadau hao kwa kuwa bega kwa bega na klabu hiyo, tangu 1992. “Tunawashukuru sana kwa kuwa nanyi mara zote inatia faraja kwetu na tutaendelea kutoa huduma bora siku zote|” alisema Mbowe.
Mtei pia aliwashukuru wafanyakazi mbalimbali waliofanikisha ukumbi huo kufikia hapo na kutoa heshima ya kipekee kwa wafanyakazi waliokuwapo tokea inaanza hadi ilipofikia miaka 20 na hatimaye kukata keki hiyo.
“Uwepo wa miaka 20, tuna kila sababu ya kuwapongeza wafanyakazi tuliokuwa nao toka mwanzo hadi leo, na kwa heshima ya pekee Mama Victor na Mrs Mitemo ndiyo watakao kata keki hii,” alisema Mtei.
Keki hiyo ilikatwa na wafanyakazi hao Monica Victor na Pili Mitemo ambaye alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo, ambaye kwa sasa ni marehemu.
Aidha, kwa upande Clouds FM, iliwakilishwa na Wasiwasi Mwabulambo ambaye alipongeza klabu Bilicanas kwa kuwa mstari wa mbele katika kuinua sanaa nchini hasa kwa kuwasaidia wasaidia wasanii kufikia malengo yao.
Kwa upande wake Ibrahim Tuwa ‘Dj Ibra’ aliyekuwa akisherehesha shughuli hiyo, aliwaomba wadau kuendelea kuwaunga mkono na wataendelea na huduma bora zaidi ha hapo. Dj Ibra alijiunga na Bilicanas tokea 2002,ambapo mpaka sasa ana miaka 10 kwenye klabu hiyo iliyowahi kuwa na madj maarufu waliopita hapo ambao wengi wao wapo kwenye vituo vya televisheni na redio.