Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Chawataka Viongozi Kupitia Kozi ya Maadili

Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa, Shadrack Mwakalila (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mipango na masuala mbalimbali ya chuo hicho. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Thomas Ndaluka.

Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa, Shadrack Mwakalila (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mipango na masuala mbalimbali ya chuo hicho. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Thomas Ndaluka.

 Mkuuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, 
Profesa, Shadrack Mwakalila.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
 
CHUO cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kimeiomba Serikali kurudisha utaratibu wa viongozi mbalimbali wa Serikali kupata mafunzo ya maadili na uongozi katika chuo hicho.
 
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi.
 
“Tulikaa na kushauriana na wenzangu ambapo tulionelea ni muhimu kuiomba serikali kurudisha utaratibu huo ili kuwanoa viongozi wetu hasa katika eneo la maadili,” alisema Mwakalila.
 
Alisema wana walimu waliobobea kitaaluma na wenye uwezo wa kutoa mafunzo hayo kwa viongozi hao na wangependa mafunzo hayo yaanze haraka iwezekanavyo.
 
Profesa Mwakalila akiongelea kuhusu mipango ya chuo hicho alisema wamejipanga kuhakikisha mipango yote iliyopangwa inakwenda vizuri hususani suala la kuongeza hosteli.
 
Alisema chuo hicho kinauhaba mkubwa wa hosteli kwa ajili ya wanafunzi ambapo baadhi yao wamepanga uraiani jambo ambalo si zuri hivyo shauku yao ni kuona wanazingongoza ili kukabiliana na changamoto hiyo.
 
Akiongelea kuhusu udahili wa wanafunzi alisema ni mzuri na kuwa unategemea na nafasi ya mwanafunzi muombaji kulingana na somo analotaka kusomea.
 
“Tunachangamoto za hapa na pale lakini kubwa ni ruzuku ndogo tunayopata toka serikalini ambayo haikidhi mahitaji ukilinganisha na mahitaji kwa mfano ikitolewa ruzuku ya sh.milioni 100 tunapata milioni 50 jambo ambalo linasabisha kukwama kiuendeshaji” alisema Mwakalila.
 
Alisema chuo hicho kilianzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 6 ya mwaka 2005 ambapo ilianza kutumika rasmi Oktoba 1 mwaka 2005 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali namba 433 la Desemba 23, 2005.
 
Alisema chuo hicho kinamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kuwa majukumu yake makuu ni pamoja na kutoa mafunzo katika fani za Sayansi Jamii kwa kiwango cha cheti, Stashahada na shahada, mafunzo ya uongozi, mafunzo ya elimu ya kujiendeleza kielimu, kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaaluma kwa sekta ya umma na sekta binafsi.