Chuo cha CBE Waibuka Vinara ‘TTCL Inter College Beach Soccer’

Wachezaji wa timu ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane Mwakalebela (wa nne kushoto) mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya fedha shs 600,000/- pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer'. CBE ilikifunga Chuo cha Ardhi mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane Mwakalebela (wa nne kushoto) mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya fedha shs 600,000/- pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Soka la Ufukweni ‘TTCL Inter College Beach Soccer’. CBE ilikifunga Chuo cha Ardhi mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.

 

Wachezaji wa timu ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya fedha shs 600,000/- pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer'. CBE ilikifunga Chuo cha Ardhi mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya fedha shs 600,000/- pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Soka la Ufukweni ‘TTCL Inter College Beach Soccer’. CBE ilikifunga Chuo cha Ardhi mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.

 

Na Mwandishi Wetu

CHUO cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE) kimeibuka vinara wa Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni ‘TTCL Inter College Beach Soccer’ yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam chini ya uratibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kupitia kocha wa taifa wa mpira huo wa ufukweni nchini.

Chuo cha CBE kilitangazwa mabingwa katika mashindano hayo na kujinyakulia kiasi cha fedha shilingi laki sita na laini za TTCL za 4G LTE, muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kukifunga Chuo cha Ardhi mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam. Mshindi wa pili katika michuano hiyo, Chuo cha Ardhi kilijipatia kiasi cha fedha shilingi laki nne pamoja na laini za TTCL za 4G LTE, muda wa maongezi wa simu na intaneti (5GB) kwa muda wa mwezi mmoja.

Awali akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Mushi kwa niamba ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba alisema kudhamini kwa mashindano hayo ni mwendelezo wa kampuni hiyo kuiunga mkono Serikali kukuza michezo anuai nchini.

Alisema TTCL inatambua kuwa michezo inamanufaa makubwa kwa jamii hasa kundi la vijana kwani licha ya kuwakinga na baadhi ya magonjwa na kudumisha ushirikiano baina yao, pia ni sehemu ya ajira ambayo imekuwa ikiwapatia baadhi yao vipato halali na kuendesha maisha yao vizuri.

 

Nahodha wa timu ya Soka la Ufukweni ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), Ally Rabi (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa timu ya Chuo cha Ardhi katika mpambano wao wa fainali ya Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' uliofanyika kwenye Ufukwe wa Coco Beach. Mchezo huo ulimalizika kwa CBE kuibuka washindi kwa magoli 2-0 na kutwaa ubingwa huo.

Nahodha wa timu ya Soka la Ufukweni ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), Ally Rabi (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa timu ya Chuo cha Ardhi katika mpambano wao wa fainali ya Mashindano ya Soka la Ufukweni ‘TTCL Inter College Beach Soccer’ uliofanyika kwenye Ufukwe wa Coco Beach. Mchezo huo ulimalizika kwa CBE kuibuka washindi kwa magoli 2-0 na kutwaa ubingwa huo.

Alibainisha michezo ina faida nyingi ikiwemo kuwafanya washiriki kuwa watu wenye afya njema ya viungo mbalimbali vya mwili, afya ya akili na uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto za maisha hivyo kujenga jamii ya watu wenye afya na furaha wakati wote jambo ambalo ni zuri kwa jamii nzima.

“…Kimsingi kwetu TTCL ni siku muhimu ambapo kwa mara nyingine, tunaungana na Wanamichezo kufanikisha tukio hili kwa udhamini wetu wenye nia ya kuithibitishia jamii kuwa kampuni ya TTCL ni mali yao, ipo kwa ajili yao na inatimiza kwa vitendo mpango wake wa kuipatia jamii huduma bora za Mawasiliano ya simu na intaneti zenye kiwango cha juu kabisa cha ubora na gharama nafuu.

“TTCL ni Wadau wakubwa wa sekta ya Michezo nchini. Wafanyakazi wa TTCL wanao utaratibu wa kushiriki michezo mbali mbali na mabonanza ya kila mara ili kujenga afya zao na kuongeza ushirikiano miongoni mwao. TTCL tunaamini kuwa, Michezo ni afya na kiungo muhimu cha mahusiano mema sehemu za kazi,” alisema Mushi akimuwakilisha Kindamba katika uzinduzihuo.

Aidha aliongeza kuwa tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa, watoto na vijana wanaoshiriki katika michezo mbalimbali katika shule zao hujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya, pombe, sigara na vitendo vya ngono ikilinganishwa na wale ambao hawajihusishi au kushiriki katika michezo, huku zikibaini wanafunzi wa kike wanaojihusisha na michezo katika ngazi mbali mbali za elimu kuwa na maendeleo mazuri ya kitaaluma jambo ambalo linapaswa kusisitizwa.

Baadhi ya vyuo vilivyoshiriki katika michuano hiyo ni pamoja na CBE, Chuo cha Ustawi wa Jamii, Chuo cha IFM, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Chuo cha NIT, DIT, TIA, Chuo cha Kodi cha TRA -ITA na Chuo cha Ardhi.