Christ Embassy Tanzania Wasaidia Watoto Yatima wa SOS Dar

Baadhi ya wahudumu wa kanisa la Christ Embassy Tanzania wakigawa zawadi mbalimbali kwa watoto wa kituo cha SOS.

Baadhi ya wahudumu wa kanisa la Christ Embassy Tanzania wakigawa zawadi mbalimbali kwa watoto wa kituo cha SOS.


Pastor Ken Igini wa Christ Embassy Tanzania akigawa baadhi ya zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha SOS Children's Villages cha jijini Dar es Salaam leo.

Pastor Ken Igini wa Christ Embassy Tanzania akigawa baadhi ya zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha SOS Children’s Villages cha jijini Dar es Salaam leo.


Sehemu ya watoto yatima wa kituo cha SOS Children's Villages cha jijini Dar es Salaam wakifurahia zawadi zao kutoka kwa kanisa la Christ Embassy Tanzania.

Sehemu ya watoto yatima wa kituo cha SOS Children’s Villages cha jijini Dar es Salaam wakifurahia zawadi zao kutoka kwa kanisa la Christ Embassy Tanzania.


Pastor Ken Igini wa Christ Embassy Tanzania akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha watoto yatima cha SOS Children's Villages cha jijini Dar es Salaam mara baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto hao.

Pastor Ken Igini wa Christ Embassy Tanzania akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha watoto yatima cha SOS Children’s Villages cha jijini Dar es Salaam mara baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto hao.


Ofisa Tawala wa Kituo cha SOS Children's Villages, Bi. Rahma Michael akizungumza kiwashukuru viongozi na waumini wa kanisa la Christ Embassy Tanzania mara baada ya kupokea zawadi hizo.

Ofisa Tawala wa Kituo cha SOS Children’s Villages, Bi. Rahma Michael akizungumza kiwashukuru viongozi na waumini wa kanisa la Christ Embassy Tanzania mara baada ya kupokea zawadi hizo.


Pastor Ken Igini wa Christ Embassy Tanzania akitoa baadhi ya zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha SOS Children's Villages cha jijini Dar es Salaam leo.

Pastor Ken Igini wa Christ Embassy Tanzania akitoa baadhi ya zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha SOS Children’s Villages cha jijini Dar es Salaam leo.


Pastor Ken Igini wa Christ Embassy Tanzania akikabidhi sehemu ya msaada waliotoa kwa kituo cha watoto yatima cha SOS Children's Villages cha jijini Dar es Salaam, anayepokea kulia ni Ofisa Tawala wa Kituo cha SOS Children's Villages, Bi. Rahma Michael.

Pastor Ken Igini wa Christ Embassy Tanzania akikabidhi sehemu ya msaada waliotoa kwa kituo cha watoto yatima cha SOS Children’s Villages cha jijini Dar es Salaam, anayepokea kulia ni Ofisa Tawala wa Kituo cha SOS Children’s Villages, Bi. Rahma Michael.


Sehemu ya watoto yatima wa kituo cha SOS Children's Villages cha jijini Dar es Salaam wakifurahia zawadi zao kutoka kwa kanisa la Christ Embassy Tanzania.

Sehemu ya watoto yatima wa kituo cha SOS Children’s Villages cha jijini Dar es Salaam wakifurahia zawadi zao kutoka kwa kanisa la Christ Embassy Tanzania.

Na Mwandishi Wetu

KANISA la ‘Christ Embassy Tanzania’ leo limekula chakula cha mchana pamoja na watoto yatima wa kituo cha SOS Children’s Villages cha jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya waumini na viongozi wa kanisa hilo wakiongozwa na chungaji wa Christ Embassy Tanzania, Ken Igini mbali ya kula chakula cha mchana na watoto hao pia walitoa zawadi mbalimbali kwa watoto wa kituo hicho. Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi zawadi hizo, Mchungaji Igini alisema wameamua kutoa msaada huo ili kuwakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwani ni sehemu ya jamii inayoitaji faraja kama ilivyo kwa watoto wengine.

Mchungaji Igini alisema msaada huo ni sehemu ya majukumu ya kanisa hilo kusaidia jamii isiyojiweza katika nyanja mbalimbali kwani wanaendesha programu nyingine ambayo ni kutoa matibabu kwa wananchi wasiojiweza na tayari imeshaanza kutekelezwa mara kadhaa.

Miongoni mwa zawadi nyingine ambazo kanisa hilo limetoa leo kwa watoto yatima wa kituo cha SOS ni pamoja na vifaa anuai vya shule, vitabu vya dini kwa watoto, sabuni za kufulia, juisi, soda, maji, biskuti, miswaki pamoja na dawa zake na vifaa vingine vidogo vidogo kwa ajili ya matumizi ya watoto.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Ofisa Tawala wa Kituo cha SOS Children’s Villages, Bi. Rahma Michael aliwashukuru viongozi na waumini wa kanisa la Christ Embassy Tanzania kwa kuwakumbuka watoto yatima hasa katika kipindi hichi cha siku kuu za mwisho wa mwaka, na kuiomba jamii nyingine kufuata mfano wa kanisa hilo kwa kuikumbuka jamii hiyo.