Muimbaji maarufu wa muziki wa kizazi kipya Chris Brown ameondolewa lawama ya wizi na kupigana na utawala wa Las Vegas Marekani baada ya mwanamke mmoja kudai alimzaba kofi na kumpokonya simu yake walipokutana kwenye Kasino moja ya kamari mapema mwezi huu.
Mkuu wa sheria katika jimbo hilo Steve Wolfson amesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kumfungulia msanii huyo mashtaka ya utovu wa nidhamu kwa kumshambulia mwanamke huyo na kumuibia simu .
Polisi walikuwa wameandikisha ripoti iliyodai kuwa Brown alimpiga mwanamke mmoja na kumpokonya simu yake alipojaribu kumpiga picha akijivinjari katika sherehe moja ya kibinafsi.
Msemaji wa Brown alikanusha madai ya mwanamke huyo akisema kuwa sio ya kweli hata kidogo.
Mwaka 2009, Brown aliagizwa kukaa miaka mitano bila kufanya kosa lolote baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga nyota wa muziki wa pop Rihanna