Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa. Elisante Ole Gabriel akikabidhiwa barua ya mwaliko wa kutembelea nchini China mwezi June mwaka huu, wakati wa mkutano baina yake na Naibu Waziri wa Habari, Utangazaji na Utamaduni wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Tian Jin (kushoto) leo jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa. Elisante Ole Gabriel (wa tano kutoka kulia) na Naibu Waziri wa Habari, Utangazaji na Utamaduni wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Tian Jin (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wakilisha Serikali za Tanzania na China wakati wa mkutano baina yao leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa. Elisante Ole Gabriel (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Habari, Utangazaji na Utamaduni wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Tian Jin alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi. Zamaradi Kawawa (kulia) akimkaribisha ukumbini Naibu Waziri wa Habari, Utangazaji na Utamaduni wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Tian Jin leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkalimani kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Bi. Karen Sunlam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa. Elisante Ole Gabriel (kulia)akimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Habari, Utangazaji na Utamaduni wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Tian Jin leo jijini Dar es Salaam. Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi.