MKUU wa Mkoa wa Tanga Luten Mstaafu Chiku Gallawa amefarijika na ugeni ambao umekuwepo jijini Tanga kwa lengo la kukabidhi miradi ya maendeleo ambayo imekamilika. Jiji la Toledo Ohio Marekani ni jiji rafiki na jiji la tanga kwa takribani miaka 10 ambapo wamekuwa wakidahmini miradi mbalimbali ya maendeleo jijiji Tanga.
Akizungumza wakati wa tafrija hiyo fupi iliyofanyika 14/02/2013, Mkuu wa Mkoa amewashukuru marafiki hao kwa ushirikiano mkubwa ambao wameuonyesha katika shughuli za maendeleo jijini. Jumla ya fedha $131367 zimetumika katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendleao ikiwemo; ukarabati wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Pongwe, wodi ya kisasa ya wazazi katika kata ya Duga na vyoo vitatu vya kisasa vya Umma katika masoko na bustani za jiji. Vyoo hivyo ni pamoja na choo katika bustani ya Sakarani na katika masoko ya Mkwakwani na Mgandini.
Wakati huo huo ametoa wito kwa wageni kuweza kufanya uwekezaji mkoani Tanga kwani ni mkoa wenye raslimali nyingi na mazingira mazuri ya uwekezaji. Ujumbe huo uliongozwa na mkuu wa msafara Bi. Norma King akiandamana na mumewe Bw. Floyd king, wazazi wa meya wa jiji la Toledo Bw. Michael bell na wajumbe wengine ni Dkt Suzan MichaelFrance amison, Althalen Harison.
Hatua hiyo ya makabidhiano ya miradi iliyokamilika ni hatua mojawapo ya mradi wa Afrika wa kudhamini miji kwa lengo la kukabilina na umasikini.Mradi unasimamiwa na TACOP (Toledo – Tanga sisters committee)
Akijibu swali ni kwa jinsi gani mradi huo umewanufaisha wananchi, Mhandisi wa jiji Eng. Gaston .P. Gesana amesema kuwa mradi huo umekuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa jiji la Tanga kwani wengi wanatumia huduma hizo na pia umekuwa ni chanzo cha ajira .