Chelsea Yasonga Mbele FA CUP, Yapiga Mtu 2-0

2510012_heroa

Chelsea imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya FA baada ya kuifunga timu ya Scunthorpe United mabao 2-0 yaliyofungwa na Diego Costa pamoja na Hazard

Mabingwa watetezi wa Kombe la FA Arsenal walitoka nyuma na kuweza kufuza kwa raundi ya tatu ya kombe hilo baada ya kuicharaza Sunderland mabao 3-1.
Sunderland ilichukua uongozi wa ghafla wakati Jeremsain Lens alipofinga akiwa nadni ya boksi baada ya beki Laurent Koscielny kufanya masihara.

Hatahivyo Arsenal ilisawazisha kupitia Joel Campbel na baadaye kuchukua uongozi kupitia bao la gusa ni guse lililofungwa na Aaron Ramsey, Baadaye mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud alifanya mambo kuwa 3-1.

2FF3C13D00000578-0-image-a-25_1452470797677

Kwengineko Sergio Aguero aliiongoza Manchester City kupata ushindi dhidi ya Norwich City, Aguero aliwachenga mabeki wa Norwich na kuiweka kifua mbele City.

2504782_heroa

Baadaye Mshambuliaji huyo aliwachenga tena mabeki wa kilabu hiyo na kutoa pasi murua kwa mshambuliaji wa Nigeria Kelechi Iheanacho aliyecheka na wavu.
City ilitawala mchezo na haikuchukua mda mrefu Kevin De Bruyne alipofunga bao la tatu.

Nayo klabu ya Manchester United alioongoza timu yake kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Sheffiled United,bao lililofungwa kwa njia ya penalti na nahodha Wayne Rooney baada ya Memphis Depay kuangushwa katika eneo la hatari.

2505892_heroa