Chelsea Yaichapa Arsenal

Nembo ya Chelsea

CHELSEA imejinyakulia pointi tatu muhimu katika kinyang’anyiro cha Ligi Kuu ya England baada ya kuilaza timu ya Arsenal magoli 2-1 katika uwanja wa Stanford Bridge leo. Juan Mata alipachika bao la kwanza la Chelsea kabla ya Frank Lampard kufunga bao la pili kupitia mkwaju wa penalti.

Hata hivyo Arsenal kupitia kwa mshambuliaji wake Theo Walcott aliweza kufunga bao zuri, akiwazidi maarifa walinzi wa Chelsea pamoja na mlinda mlango wao. Kipindi cha Arsenal ilizidi kuibana Chelsea ambapo ilipata kona tisa dhidi ya tatu za Chelsea. Hata hivyo mechi hiyo ilimalizika kwa Chelsea kuibuka na ushindi huo wa magoli mawili kwa moja.

Huu ni ushindi wa kwanza kwa Chelsea katika uwanja wake mwaka huu 2013 kati ya mechi nne ilizocheza uwanjani hapo Stanford Bridge. Ratiba ya mashindano ya kandanda ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2013 nchini Afrika Kusini. Tarehe 19 Januari hadi 10 Februari.

-BBC