Na; Woinde Shizza ,Arusha
Mahabusu ya watoto jijini Arusha inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa huduma za kiafya ikiwemo madawa pamoja na muhudumu wa afya anaehudumia watoto waliopo katika mahabusu hiyo.
Ayo yamebainishwa jana na Afisa ustawi wa jamii ambaye pia ni misimamizi wa mahabusu ya watoto Mussa Mkamate wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada wa magodoro 25 kutoka kwa jumuiya ya wazazi wa CCM wialaya ya Arusha .
Alisema kuwa mahabusu hiyo ya watoto imekuwa ikisumbuliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ukuta wa mahabusu ,ukosefu wa walinzi wa mahabusu hao ambao ni watoto hali ambayo inasababisha wakati mungine watoto hao kuweza kutoroka katika mahabudu hiyo.
Mbali na hayo pia afisa ustawi wa jamii hiyo aliitaka serekali kuweza kusaidia mahabusu hiyo kuwa na vitendea kazi ikiwemo usafiri wa watoto wao pindi wakiwa wanaumwa gafla pamoja na pale wanapopelekwa mahakamani kwani alibainisha kuwa muda mungine iwapo mahabusu motto anapoumwa viongozi ambao waliopo katika mahabusu hiyo wanalazimika kutoa fedha mifukono kwao na kukodisha usafiri kwa ajili ya kumpeleka mtoto huyo hospitalini.
“pia kumekuwa na tatizo kubwa la ucheleweshaji wakusikiliza kesi za
hawa watoto unakuta mtoto amekaa mahabusu kwa muda mrefu na kesi yake aisikiliswi pia napenda sana kuiomba serekali itusaidie kuarakisha kesi hizi za hawa watoto ili ziweze kusikilizwa kwa haraka na kwa wakati “alisema Mussa
Aliongeza kuwa pia wamekuwa wanakutana na changamoto ya kutokuwepo kwa mahakimu wa kusikiliza kesi za watoto hali ambayo inalazimu kesi hizi za watoto kusikilizwa katika mahakama ya mwanzo ambapo muda mungine mahakimu waliopo katika mahakama hizi za mwanzo wamekuwa wakitoa hukumu pasipo kumuangalia umri wa mtoto.
“kama ivi kati kuna mtoto kashtakiwa kakubali kosa baada ya kukubali
kosa kahukumiwa miaka miwili na mtoto huyo anaumri wa miaka 12 mbali na ivyo ikirudi kwenye katiba au sheria ya nchi hairuhusu motto kuhukumiwa kifungo anatakiwa kupewa adhabu sasa hii inaumiza sana sasa tunaomba serekali angalau ianzishe mahakama ya watoto ili kuweza kutatua tatizo hili kwani bila kufanya hivyo itapelekea kuendelea kuwaumiza watoto wetu hawa ata kama wanamakosa”alisema Musa.
Kwa upande wake mjumbe mmoja wa Jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Arusha ambaye pia ni afisa masoko wa Radio Triple A Fm iliopo mkoani Arusha Phidecia Mwakitalima aliiomba serekali kuweza kusadia kuongeza maafisa ustawi wa jamii ambao wataenda na watoto hao mahakamani kuwasikilizia kesi zao na kubainisha kuwa iwapo maafisa ustawi watakuwa wengi basi inaweza kusaidia pia hata hawa watoto kupata hakizao za kimsingi wanapopelekwa mahakamana na hata pale wanapokuwa mahabusu.