Dk. Chami afungua maonesho ya wajasiriamali Mbinga

Wakwanza (mrefu) Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Mike Laizer, wapili ni Dk. Cyril Chami, Waziri wa Viwanda na Biashara akifuatiwa na Dk. Christine Gabriel Ishengoma, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na mwenye shati la kitenge ni Gaudence Kayombo, Mbunge wa Mbinga Mashariki (Picha na Dunstan Mhilu.

Na Dunstan Mhilu, Mbinga

MAONESHO ya wajasiriamali wadogo na wakati Kanda ya Kusini yamefunguliwa rasimi na Waziri wa Viwanda na Biashhara Dk. Cyril Chami katika  viwanja vya CCM wilayani Mbinga.

 Akizungumza na wajasiriamali hao pamoja na wakazi wa mbinga   aliwapongeza kwa ukarimu wao  wa kukarimu wageni nakuipongeza SIDO Mkoa wa Ruvuma kwa kufanikisha maonesho hayo.

 Aidha amewataka wana mbinga na kanda ya kusini kutumia fursa zilizopo katika mikoa hiyo na siyo kusubiri watu watoke nje ya kusini waje wawekeze wakati wao wana uwezo wakuwekeza.

   “Mbinga mna uchumi mzuri pamoja na mikoa ya kusini tumieni fursa ya  rasilimali zinazo patikana katika ukanda huu ili kujimarisha kiuchumi,mna Aridhi nzuri yenye rutuba na madini ya kutosha, ni hivi karibuni madini yatachimbwa hivyo basi lazima ya waboreshee maisha.”

 Ameongeza kuwa ni aibu kuona watu wakutoka mbali walete mayai, nyama Ruvuma wakati wakazi wa mbinga wana uwezo huo. Hata hivyo amewataka wajasiria mali hao kutumia fursa ya soko la afrika mashariki ambapo soko hilo linazidi kuwa kubwa kutokana na nchi za Sudani ya kusini, Sudani Kaskazini, na Rwanda kuomba kujiunga na Jumuia ya Afrika Mashariki.

Mkurugenzi mkuu wa SIDO, Mike Laizer alimueleza mheshimiwa waziri kuwa pamoja na wajasiriamali hao kuwa pamoja na wajasiriamali hao kupata mafunzo mbali mbali yakibiashara na usindikaji kutoka SIDO lakini kuna mradi wa Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI).

 Mradi huu upo katika mikoa sita ikiwemo Ruvuma ambao wana wawezesha wajasiriamali wanao jishughulisha na mazao ya mhogo na alizeti wamefanikiwa kuviwezesha vikundi kumi na nne vilivyopo wilaya ya Mbinga, Namtumbo na Songea Vijijini.

 Naye mratibu wa mradi wa MUVI Ruvuma na Mwanza Bw Salum Lupande alimueleza mheshimiwa waziri kuwa mradi huo una imarisha mnyororo wa thamani ili kuongeza kipato na kupunguza umasikini.

 (Picha, habari na Dunstan Mhilu)

.