Chama cha Bodaboda Liwale Chakopesha Pikipiki 62 kwa ‘Bodaboda’

Chama cha Bodaboda Liwale Chakopesha Pikipiki 62 kwa 'Bodaboda'

Chama cha Bodaboda Liwale Chakopesha Pikipiki 62 kwa ‘Bodaboda’

Wilson Nyamanga

Mgeni rasmi akikabidhi pikipiki kwa mwanacha hii leo maeneo ya ofisi za chama cha bodaboda.
Mary Ding'ohi

Afisa maendeleo ya jamii wilayani Liwale bibi Mary Ding’ohi akifafanua jambo.
 
Na Mwandishi Wetu, Liwale

CHAMA cha waendesha bodaboda wilayani Liwale mkoani Lindi kimetoa mikopo ya pikipiki kwa wanachama wake wapatao 62 zenye thamani ya shilingi 92,000,000.

Chama hicho kilipata mkopo wa pikipiki 20 zenye thamani ya shilingi 35,000.000/= kutoka mfuko wa Maendeleo ya Vijana wa Wilaya na kuweza kukopeshwa kwa mwanachama mmoja mmoja na kupitia umoja wao chama kiliweza kupata pikipiki 42 na kuweza kufikia ya jumla ya pikipiki 62.

Leo wamekabidhi pikipiki mbili kwa wanachama wawili zenye thamani ya shilingi 4,400,000/= na kukabidhi kwa mwanachama mmoja bati zenye thamani ya shilingi 2,000,00/= jumla ni 6,400,000/= na wameweza kufanya marejesho ya shilingi 6,325,000/=.

Chama hicho  Kina miaka Sita Tangu kuanzishwa kwake Mnamo mwezi Mei mwaka 2010 kikiwa na waanzilishi 65 pia chama hicho kinatambuliwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Liwale na kimepatiwa Hati ya Utambulisho Mwaka 2014.

Kwa sasa chama kina jumla ya wanachama 300 wenye sifa na vigezo vinavyokidhi mahitaji ya katiba na vigezo vinavyotumika kumkopesha mwanachama ni awe mwanachama hai na awe na kiwango cha hisa cha mwanachama.

Pamoja na mafanikio hayo yaliyopatikana zipo changamoto zinazowakwamisha kushindwa kutekeleza malengo yao, changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa fedha za kuendesha ujenzi wa ofisi pamoja na uwepo wa mtaji mdogo ambao unakosesha kuwakopesha pikipiki wanachama wengi kwa wakti mmoja.

Akikabidhi pikipiki hizo mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya bwana Wilsoni Nyamanga ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya Liwale amewataka waendesha pikipiki hao kuwa na umoja kwani katika umoja huo kutasaidia kutatua changamoto mbalimbali.
“Katika umoja wenu imekuwa ni chanzo cha ajira na tunatambua wengi wenu mumeepuka kujihusisha na vitendo viovyu vya kunyang’anya na kukaba pia sisi kama watu wa ulinzi na usalama kwetu ni faraja na kama serikali tumewatambua kama wadau wa maendeleo” alisema Nyamanga.

Hata hivyo katibu tawala huyo amewasisitizia kuzingatia sheria na taratibu walizojiwekea katika katiba yao na kufanya maamuzi yanayoendana na malengo yao kwa kutaka kuwepo kwa viongozi bora na wa demokrasia ambayo mambo yote yanayofanyika yanakuwa ya wazi na shirikishi kwa kupeana taarifa mbalimbali na kuweza kuweka malengo makubwa na kuweka malengo yanayotekelezwa kwa kikomo.

Mmoja wa wanachama waliokabidhiwa pikipiki hizo leo Rajabu Kyula alisema amejisikia furaha sana kukabidhiwa pikpiki kwani mwanzoni alikuwa na pikipiki ya Bosi na sasa imekuwa mwokozi kwani sasa malengo yake yatakuwa yametimia na ataweza kukuza kipato chake pia amewashauri watu wengine kuweza kujiunga na chama hicho waweze kunufaika na mpango huo wa kukopeshana pikipiki.

Pia Idi Rashidi alisema amejiskia vizuri kukabidhiwa pikipiki na amewashauri watu wengine kujiunga na chama cha bodaboda kwani chama hicho kimekuwa mkombozi wa vijana wengi hapa wilayani.

Mwenyekiti wa chama hicho Rafii Kikochelo alisema amewawezeshaa wanachama wake kuwakabidhi pikipiki na bati na kwa msaada huu imewawezesha zaidi ya familia ya watu wanne watanufaika na mpango huu kwa wale waliojiunga na jitihadi zaidi ya kutafuta mkopo wa zaidi ya pikipiki 30 au 50 Kwa benki ya CRDB zinafanyika na hatua mzuri imefikia ya kukopeshwa kwa lengo la kuwapatia wanachama wengi kuweza kupata mkopo kwa wale wanachama hai ambao wanalipa ada ya wanachama kwa mujibu wa katiba.