MBUNGE wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Rejea Mtema amefariki dunia leo asubuhi kwa ajali mkoani Pwani.
Taarifa ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba Mbunge Mtema amefariki dunia papo hapo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupinduka, lilipomshinda akilipita gari lingine eneo la Ruvu mkoani Pwani.
Mtema ambaye alikuwa akielekea mjini Morogoro kutokea Dar es Salaam inasemekana ndani ya gari hilo alikuwa na abiria wengine wanne ambao wanatibiwa katika Hospitali ya Tumbu Pwani.
Taarifa zaidi tutawaletea hapo baadaye baada ya kuzipata kwa kina. Mtandao huu unatoa pole kwa Uongozi mzima na Wanachama wa CHADEMA pamoja na familia, ndugu, jamaa wa Mbunge Mtema.