Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI, Katibu na Muweka hazina, wa Jumuia ya Watanzania waishio Marekani, wanashutumiwa na Wanajumuia wa Washington kuwa wamepokea Rushwa kutoka kwa Chadema kwa ajili ya kufanyia picnic na party ya Usiku, vitakavyofanyika Agosti 25, 2012.
Habari za madai za Shutuma hizo zinasema kuwa Jumuia ilikuwa na Fedha taslim zisizozidi Dola 2000 za Marekani zinazotosha kufanya party ya mchana ya picnic peke yake, lakini cha kushangaza wakati Wanajumuia wakiwa wanahoji kwa nini party ya usiku ifanyike wakati Jumuia haina fedha za kutosha, Viongozi hao wameweza kuja na fungu kubwa la fedha ambazo watazitumia kufanya party zote mbili kubwa za kifahari zitakazoambatana na Chakula na vinywaji Mchana na Usiku bure.
Kama haitoshi kutokana na fungu hilo, Pombe zitakuwa za bure hadi saa Nane usiku, wakati Ukumbi na Muziki vikiwa vimelipiwa kwa Cash siyo Mkopo.
“Habari za kuaminika na ushahidi upo zinasema kuwa Katibu wa Jumuiya Bwana Amosi Cherehani ni Muweka Hazina wa Chadema Washigton na ndiye ambaye ameweza kuhamasisha Fedha hizo kutoka Chadema iliziweze kufanya hafla hiyo”, Imesema taarifa iliyotumwa kwa Mtandao kutoka Marekani.
“Wananchi wanahoji kwa nini Mwenyekiti ambaye alichaguliwa kwa kishindo ameweza kukubali kadhia hii wakati Jumuiya haifungamani na Chama chochote cha siasa?” Imehojiwa katika taarifa hiyo.
“Kutokana na kadhia hiyo, wakereketwa wa Jumuiya wameipa Mamlaka Kampuni ya ERNEST & YOUNG kufanya “INDEPENDENT AUDITING” ya Jumuiya ili kujua “INCOME AND EXPENDITURE za Jumuiya yao zimetoka wapi na zimetumika vipi kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa”, Taarifa imesema.
Tarifa imesema wanajumuiya wanaomba kuitisha Mkutano ili kupiga Kura za maoni ya kutokuwa na Imani na Uongozi kwakuwa bado mchanga. ..”Na tuliuchagua kwa Imani, hatutaki vyama vya siasa vituingile…Rushwa ni adui wa Haki”