Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akisalimiana na Viongozi na wanachama wa CCM, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, nje ya Mji wa Zanzibar akitokea Mkoani Dodoma,katika Mkutano Mkuu wa nane wa Chama hicho uliomuwezesha kushika nafasi hiyo,baada ya kushinda uchaguzi kwa kishindo.
Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akivalishwa shada la mauwa na mtoto Salama Issa Ali, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea Mkoani Dodoma,kulikofanyika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliomuwezesha kushika nafasi hiyo,baada ya kushinda uchaguzi kwa kishindo.
Wanachama wa CCM waliojitokeza kumpokea Makamo wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakiwa wamejipanga kwa mistari na wengine kubeba mabango ya Majimbo katika mtaa wa Michenzani kuelekea CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Maandamano ya Pikipiki kama yanavyoonekana pichani wakiongoza msafara wa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akitokea Dodoma katika Mkutano Mkuu wa Nane,ulimuwezesha kushika nafasi hiyo katika uchaguzi,wa kuwachagua Viongozi wa CCM kwa kipindi cha miaka mitano,katika ukumbi wa Kizota, Mkoani Dodoma.[Picha zote na Ramadhan Othman Ikulu.]