CCM Yavuna Wanachama 180 Mkutano wa Hadhara Mtwara

Umati wa wananchi pamoja na wanaCCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) katika viwanja vya Manispaa ya Mtwara Mikindani.

 Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi pamoja na wanaCCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Manispaa ya Mtwara Mikindani leo.

Baadhi ya wasanii wakiburudisha umati wa wananchi pamoja na wanaCCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni  wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Manispaa ya Mtwara Mikindani leo.
Sehemu ya umati wa wananchi pamoja na wanaCCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) katika viwanja vya Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Mmoja wa viongozi wa CCM Mtwara Mjini akiwakaribisha wageni na kufungua mkutano wa kampeni.
Sehemu ya meza kuu kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika viwanja vya Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Mgomgea ubunge wa Jimbo la Mtwara Mjini, Murji Hasnain Mohamed akiwahutubia wananchi pamoja na wanaCCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara, Mohamed Sinani akizungumza na wananchi pamoja na wanaCCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan.   Na Joachim Mushi, Mtwara   MKUTANO wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi    (CCM), Bi. Samia Hassan Suluhu umefanikiwa kuvuna wanachama 180 kutoka vyama    mbalimbali vya upinzani Mkoani Mtwara.   Katika mkutano huo uliofanyika leo Manispaa ya Mtwara Mikindani jumla ya wanachama    180 kutoka vya CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi, TLP na ACT Wazalendo wamerudisha kadi    zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi ambapo wamepokewa na Bi. Samia Suluhu.   Akizungumza katika zoezi la kuwapokea wanachama hao wapya mgombea mwenza Bi. Suluhu    aliwaomba wanachama wa CCM Mtwara kuwapokea vijana hao na kuwatumia kufanya kazi za    kampeni kwani wamerudi nyumbani hivyo hakuna haja ya kuwatenga.   Akimnadi mgombea wa urais wa chama hicho, Dk. John Pombe Magufuli, Bi. Suluhu    aliwaomba wanaMtwara kumpigia kura mgombea huyo kwani ana mambo makubwa aliopanga    kuyafanya kwa Mji wa Mtwara ili kuhakikisha unakuwa kiuchumi pamoja na wananchi    wake.   Alisema Serikali ya CCM imepanga kujenga reli itakayotoka Mtwara kwenda Songea hadi    Mbambabay ambayo itakuwa mtaji mkubwa kiuchumi wa viwanda kwa mkoa huo, kwani    itakuwa ikisafirisha makaa ya mawe kutoka Songea Mkoani Ruvuma kuja katika viwanda    vitakavyojengwa Mkoa wa Mtwara.   Aliongeza kuwa wamepanga kujenga maegesho ya meli kubwa manne mkoani Mtwara hatua    ambayo itaongeza ukubwa wa Bandari na wingi wa meli zitakazokuwa zikiingia na    kutoka mkoa humo jambo ambalo alisema litachangia kukuza uchumi wa nchi hiyo.   Aliongeza kuwa watahakikisha wananchi ambao viwanja vyao vimechukuliwa kwa ajili ya    shughuli nyingine katika maeneo ya Magomeni, Ufukweni, Matengo pamoja na Mji Mwema    wanalipwa fidia kulingana na soko la sasa.   Alisema Serikali ya CCM inapigana na umasikini na sio masikini hivyo lazima    iendelee kuwalipa vizuri wananchi ambao viwanja vyao vimetwaliwa kwa shughuli    nyingine. “…Tunapigana na umasikini wala si masikini, lengo ni kuwawezesha,”    alisema Bi. Samia Suluhu.   Mgombea huyo mwenza leo anamaliza ziara yake ya kuinadi ilani ya Chama Cha    Mapinduzi mikoa ya kusini ambapo alipita majimbo ya Mikoa ya Lindi na Mtwara    kuelezea nini watawafanyia wananchi wa maeneo hayo endapo watapata ridhaa ya kuunda    dola tena. 
Baadhi ya vijana wakiwa wamepanda juu ya miti kushuhudia matukio katika mkutano wa kampeni wa CCM Mtwara Mjini.
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM, Bi. Hawa Ghasia akiwa amempakata mtoto kwenye mkutano huo wa kampeni.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwapokea wanachama wapya wa CCM waliohamia kwenye mkutano wake wa kampeni Mikindani Mtwara.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwapokea wanachama wapya wa CCM waliohamia kwenye mkutano wake wa kampeni Mikindani Mtwara.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (katikati) akipokea kadi toka kwa wanachama wapya wa CCM waliohamia kwenye mkutano wake wa kampeni Mikindani Mtwara.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (katikati) akionesha kadi alizopokea toka kwa wanachama wapya wa CCM waliohamia kwenye mkutano wake wa kampeni Mikindani Mtwara.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com