CCM Yapokea Makatibu Wakuu Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika

1. Dr Migiro akimpokea Ai Ping wa CPC cha China
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, akimlaki Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Jamhuri ya watu ya China Ai Ping baada ya mgeni huyo kuwasili mchana huu Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo. Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) ambacho ni rafiki mkubwa wa CCM kimealikwa kutokana na kuwa Chama kilichosaidia sana harakati za ukombozi huo wa nchi za kusini mwa Afrika. Katikati ni Balozi wa China hapa nchini, Lu Youqing.

2. Dk. Asha-Rose akizungumza na Ai Ping
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, akizungumza nai Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Jamhuri ya watu ya China Ai Ping baada ya mgeni huyo kuwasili mchana huu Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo. Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) ambacho ni rafiki mkubwa wa CCM kimealikwa kutokana na kuwa Chama kilichosaidia sana harakati za ukombozi huo wa nchi za kusini mwa Afrika. (Picha na Bashir Nkoromo).
1(5)

 

Dk. Asha-Rose Migiro, akimlaki Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Jamhuri ya watu ya China Ai Ping baada ya mgeni huyo kuwasili mchana huu Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

CHAMA CHA MAPINDUZI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Leo Jumatatu tarehe 07/10/2013 Chama cha Mapinduzi kinapokea ugeni mkubwa wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Makatibu Wakuu hawa wanakuja kuhudhuria Mkutano wa Sita ambao ni mwendelezo wa mikutano ya aina hii inayofanyika mara mbili kwa mwaka.

Vyama vyote vya Ukombozi vitahudhuria Mkutano huu utakaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 09 Oktoba. Vyama hivyo ni ANC cha Afrika ya Kusini; FRELIMO cha Msumbiji, MPLA cha Angola; SWAPO cha Namibia; ZANU-PF cha Zimbabwe na Chama mwenyeji CCM.

Mkutano wa Makatibu Wakuu utatanguliwa na mikutano ya Jumuiya za Vijana, Wanawake na Maveterani itakayofanyika Jumanne Oktoba 8, 2013.

Mkutano wa Sita wa Makatibu Wakuu utahudhuriwa pia na ujumbe kutoka Chama rafiki cha Kikomunisti cha China utakaoongozwa na Ndugu Ai Ping, ambaye ni Naibu Waziri anayeshughulikia Idara ya Kimataifa ya Chama hicho.

Pamoja na mambo mengine Mkutano huu wa Sita wa Makatibu Wakuu wa vyama vya Ukombozi kusini mwa Afrika utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa katika kikao chao cha tano kilichofanyika huko Tshwane, Afrika ya Kusini mwezi Machi, 2013.

Mojawapo ya maazimio hayo ni ujenzi wa Chuo cha Pamoja cha Vyama hivi vya Ukombozi utakaofanyika Ihemi, katika mkoa wa Iringa. Makatibu Wakuu wanatarajiwa kuzuru eneo la Ihemi tarehe 08/10/2013 kama sehemu ya maandalizi ya majadiliano ya Mkutano huo wa Sita.

Mkutano huu utafunguliwa rasmi na Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi tarehe 09/10/2013.

Imetolewa na :-

Asha-Rose Migiro
KATIBU WA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA
CHAMA CHA MAPINDUZI
07/10/2013