CCM Yalaani Kipigo cha Mhariri Mtanzania, Yaitaka Serikali Kuwasaka Wahusika

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda usiku wa kuamkia Jumatano Machi 6, 2013.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye; amesema Chama Cha Mapinduzi kinalaani kwa nguvu zote kilichotokea kwa Absalom Kibanda, kwani ni unyama usiokubalika hata kidogo, unafaa kulaaniwa na Watanzania wote.

“CCM tunaitaka Serikali kuhakikisha inawapata waliofanya unyama huo na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake, na kukomesha matukio ya namna hiyo,” alisema Nape.

Aidha, Chama Cha Mapinduzi kimetoa pole kwa Uongozi wa Jukwaa la Wahariri, Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006, familia ya Ndugu Kibanda, wanahabari na wadau wote wa habari nchini, na tunamwombea kwa Mwenyezi Mungu apone haraka na kurejea katika kazi zake za Ujenzi wa Taifa.