TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa Agosti 21, 2012 na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora. Kimejiridhisha na kufanya uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga mkoani Tabora Dokta Dalaly Peter Kafumu.
Kusudio hilo linatokana na kutorishwa na hukumu hiyo.
Imetolewa na;-
Nape Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM
WA ITIKADI NA UENEZI
22/08/2012