
Msimamizi wa uchaguzi wa kura za maoni uliofanywa na wabunge kuwapata wagombea wa ubunge wa Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM, Abdulrahman Kianana akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa kikao cha uchaguzi huo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, jana.

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kukanusha kuhusika na kashfa ya mradi wa machinjio ya kisasa jijini Dar es Salaam, Kama ilivyoripotiwa na gazeti moja la kila siku.