Alisema uzalishaji wa zao hilo kwa sasa inafanya vizuri hivyo endapo Serikali ya CCM itafanikiwa kushinda uchaguzi wa mwaka huu itafanya mazungumzo na nchini ya China na kuanza kuwauzia zao hilo kwa kuwa wanalihitaji kwa matumizi.
Alisema lengo la Serikali ni kuboresha kwanza mazingira ya kilimo cha korosho eneo hilo ili kiweze kuwanufaisha wakulima kwa kuongeza pembejeo, zana za kilimo pamoja na ruzuku anuai kwenye uzalishaji wa korosho, lakini kwa kuwa zao la muhogo pia linazalishwa katika baadhi ya maeneo hayo Serikali itafanya mazungumzo kuweza kupata soko nchini china.
“…Suala la kilimo cha mihogo tutatafuta soko lake nchini China, endeleeni kuzalisha muhogo unaokidhi mahitaji,” alisema mgombea mwenza Bi. Suluhu.
Bi. Samia kesho anatarajia kuanza ziara yake ya kuinadi ilani ya CCM katika majimbo anuai ya Mkoa wa Tanga na baadaye Morogoro kabla ya kuingia Mjini Dodoma, akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya kampeni kitaifa ya chama hicho.