Na Mwandishi Wetui, Arusha
WAJUMBE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Arumeru leo wamelazimika kuondoka mkutanoni baada ya kukerwa na kitendo cha uamuzi wa kupewa nafasi mtoto wa Jeremiah Sumari, Siyoi Sumari, kugombea Jimbo la Arumeru Mashariki alioliacha baba yake aliyefariki hivi karibuni.
Minong’ono imeibuka kuwa kitendo cha kupewa mtoto huyo ni ishara ya kuliachia Jimbo lichukuliwe na CHADEMA, huku wakidai kufanya hivyo pia ni kuendkeza kurithishana madaraka.
Baadhi ya wajumbe waliozungumza na mtandao huu jana kwa nyakati tofauti nje ya Ukumbi wa Tareto ulioko Arumeru Mashariki, baadhi ya wajumbe hao walidai kuwa wamesikitishwa na matokeo hayo ambayo yamempa ushindi Siyoi aliyeshinda kwa kura 361 kati ya wapiga kura 1034.
“CCM ilipaswa kutafakari kabla ya kumpitisha mtoto huyo wa marehemu katika picha ya jamii ya kabila la Meru, ni mbaya kwa sababu inaonyesha Jimbo hili kwa sasa limegeuzwa kuwa la Kifalme, ila wasitupe lawana pale tutakapowapa Chadema kura, kwani kupitishwa kwa Siyou kunazua utatamkubwa kwani kulikuwa na umwagaji wa fedha kama njugu, wagombe aambao hawakutoa fedha ndiyo walioanguka” alilalamika mmoja wa wajumbe wa mkutano huo.
Katika uchaguzi huo uliochukua ya saa zaidi ya saba na kumtangaza mshindi saa tatu kasoro usiku, wagombe wa nafasi hiyo walikuwa ni Siyoi Sumari aliyeibuka kiedea kwa kupata kura 361, William Sarakikya 259, Elirehema Kaaya aliyepata 205, Elishiria Kaaya 176, Anthony Msani 22 na Rishiankira Urio kura 11.
Mmoja wa wagombea hao Anthony Musani, ambaye pia ni Mwalimu Mkuu Shule ya Sekondari Leguruki, akizungumzia uchaguzi huo na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alidai kuwa uchaguzi huo haukuwa huru wala wa haki kwani rushwa ilitawala.
Alidai kuwa baadhi ya wagombea walibebwa na viongozi wa kamati za siasa hivyo haki ilikuwa ni vigumu kuweza kutenda, huku akidai kuwa kulikuwa na kila aina ya uchakachuaji kwa sababu kura zilimazlizika kupigwa saa 11. 00 jioni na badala ya kutengaza mshindi wakachelewesha hadi saa tatu kasoro na kumtangaz mshindi waliokuwa wakimtaka.
Alidai kuwa viongozi wa CCM mkoa na Wilaya waliifahamu juu ya kuwepo kwa vitendo vya rushwa ila walifumbia macho suala hilo pasopi kuchukua hatua yoyote, na kuongeza kuwa anaandika barua ya malalamiko ya kutoridhika na uchaguzi huyo na kupeleka katika Kamati ya siasa ya Mkoa na Wilaya.