Na Fredy Mgunda, Iringa
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa HASSANI MTENGA, amefungua rasmi kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa katika Mtaa wa Semtema mkoani iringa. Akiwahutubia mamia ya wananchi wa mtaa wa semtema MTENGA aliwataka wananchi wa eneo hilo kuwa makini wakati wa kuchagua kiongozi katika uchaguzi utakao fanyika tarehe 14/12/2014.
MTENGA alisema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi na watu binafsi kwa kuwa kila maendeleo yanaanzi chini ndio yanaenda juu, hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini sana na kumchagua kiongozi anayefaa.
Aidha MTENGA aliwataka wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa kuacha kuiga siasa chafu ambazo waiga kutoka kwa wapinzani wao kwa kuwa wanaiga kitu ambacho hawakijua ambacho kitawaletea madhara baadae.
Alisema kuwa IRINGA ni ya watu wa iringa hivyo kuwaambia wanafunzi wa vyuo vyote mkoani iringa kuwaachia siasa wana iringa na wao waendelee na walicho kifuata hapa na sio isasa.
Kwa upande wake wanafunzi waliohudhuria mkutano huo walimsifu katibu huyo wa chama cha mapinduzi kwa kuwa na sera zinazotekeleza na kuwaambia ukweli vijana waliopo vyuoni kwqa kuwa wananfunzi wengi wamekuwa wakiiga mambo mengi bila kujua nini kipo mbele yao.
Lakini wananchi waliojitokeza eneo hilo walimuita katibu huyo kwa jina dawa ya muarobaini kwa maneno aliyoyatoa katika mkutano huo na kumsifu kiongozi huyo kuwa ni kiongozi ayefaa kuigwa hapa mkoani iringa.
Pia kunabaadhi ya wananchi walisikika wakisema kwa sera za katibu MTENGA mbunge wa Jimbo la Iringa mjini atake asitake ataondoka tu na kumwomba aanze kukusanya kilicho chake.