Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kushoto) akiosha moja ya magari ya wabunge na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) kuwaunga mkono waandishi wa habari katika tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari …
Media Car Wash yaanza kwa mafanikio Dodoma
Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja akisalimiana na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani wakati wa harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. …
Harambee ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari Kufanyika Dodoma Juni 25
KAMATI ya Maandalizi ya tukio la Okoa Maisha ya waandishi wa habari, imeandaa harambee maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016. Lengo la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi wa habari takribani 1000 hapa nchini. Kamati …
Dk. Regnald Mengi Achangia Madawati 1,000
KATIKA kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuhakikisha tatizo la madawati nchini linamalizika hadi kufikia Juni, 30 mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa Mashirika ya IPP, Dk. Reginald Mengi ametoa msaada wa milioni 70 kwa wilaya ya Handeni, Tanga na Bagamoyo, Pwani kila moja ikipata milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 1,000 ambayo yatasaidia kumaliza tatizo hilo katika …
Ubia wa TTCL na Bharti Airtel Wafikia Kikomo
Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Profesa Tolly Mbwete (katikati) hati ya mauzo ya hisa asilimia 35 za Kampuni ya Bharti Airtel Afrika. Serikali imezinunua rasmi hisa za kampuni hiyo ndani ya TTCL ambapo leo wamesaini mkataba wa mauziano wa hisa hizo. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel …
Rais Dk Magufuli Ahudhuria Maadhimisho ya Miaka 50 ya Benki Kuu Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli akizindua sarafu maalumu ya shilingi 50,000/- kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa Benki kuu (BOT) jijini Dar es salaam jana Juni 22, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na kumkaribisha aliyekuwa Makamu wa …