Mkutano wa Shukrani na Kuombea Tanzania Kitaifa Kufanyika Jumamosi

    Na Dotto Mwaibale   MRATIBU wa mkutano wa kitaifa wa kuombea nchi na Rais Dk.John Magufuli, ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Abudant Blessing Center (ABC), Askofu Flaston Ndabila amesema viongozi wa Serikali, kidini na wananchi watakutana kesho kutwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam katika maombi maalum ya shukrani ya kuiombea nchi pamoja na Rais Dk. John …

Makamu wa Rais, Samia Amrithi Mama Salma Kikwete TGGA

  Aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mama Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan bendera ikiwa ni ishara ya kumpatia ulezi wa chama hicho katika hafla iliyofanyika, kwenye viwanja vya Jumba la Makumbusho Dar es Salaam leo .  Samia Suluhu Hasan akimkabidhi Mlezi mstaafu wa TGGA zawadi ya saa aliyopewa zawadi na uongozi …

Waziri wa Ujenzi, Prof. Mbarawa ‘avamia’ mradi wa barabara za juu Tazara Dar

    WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa leo amevamia mradi wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam na kuridhishwa na kasi ya ujenzi inayoendelea chini ya Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd ya nchini Japan. Akizungumza katika ziara hiyo alisema lengo ni kuangalia maendeleo ya ujenzi …

Katibu Mkuu Kiongozi, Kijazi Aongoza Mazishi ya Hassan Rashid Shebuge

  KATIBU Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Jumamosi Julai 6, 2017 ameongoza waombolezaji wakiwemo ndugu, jamaa, marafiki, majirani na wafanyakazi wenzie katika mazishi ya aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyefariki dunia siku ya Alhamisi, Julai 6, 2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupatwa na shinikizo la damu. Marehemu Shebuge, …

Rais mstaafu Kikwete azindua Tamasha la ZIFF 2017 Zanzibar, Atunukiwa tuzo

  RAIS Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi usiku wa Julai 8,2017, amezindua rasmi tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), tukio lililofanyika Ngome Kongwe, Mjini Unguja-Zanzibar. Katika tukio hilo, Dkt. Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo la 20, tokea kuanzishwa kwake miaka …

SIKU YA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI YAFANYIKA KITAIFA DODOMA

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama Taifa (Mwenye T-Shirt ya Blue) akiwa ameambatana na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini DCP Mohammed Mpinga ambae pia ni katibu wa Kamati ya usalama barabarani na Mlezi wa RSA Tanzania wakiwa wanaingia uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma baada ya kupokea maandamano ya …