Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Rebeca Mongy akizungumza juu ya mipango waliyonayo kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kulia Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii Jiji la Arusha, Tajiel Mahega. Mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii Jiji la Arusha, Tajiel Mahega akizungumza katika mkutano huo. …
Vijana Tumieni Fursa Zilizopo Kujiajiri-Serikali
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Leornad Akwilapo amewataka vijana kutafuta ajira sehemu mbalimbali kwa kutumia fursa zilizopo badala ya kutegemea fursa za serikali. Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, iliyolenga kuweka mkakati wa pamoja kati ya wadau …
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Ladhamini Rock City Marathon
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dk. Leonard Masale (kushoto), akiwa pamoja na baadhi ya waandaji na washiriki wa mbio za Rock City Marathon katika viwanja vya CCM jijini Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (katikati) akiwa na mwanariadha wa zamani, Juma Ikangaa (kulia), na washiriki wengine wa mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza juzi na kudhaminiwa na Shirika la …
Sumatra Waja na Mpango wa Kupambana Uchafuzi Mazingira Baharini
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) Captain Mussa Mandia, katikati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuzungumzia mpango maalumu wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, kushoto ni Meneja Mawasiliamo wa Sumatra, David Mziray kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud. …
Mtendaji Mkuu Mpya wa TTCL Atembelea Ofisi Yake
KAIMU Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba, leo ametembelea Makao Makuu ya TTCL na kukutana na Mtangulizi wake, Dk. Kamugisha Kazaura. Utambulisho wa awali wa kiongozi huyo mpya umefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, anaesimamia sekta ya Mawasiliano Prof Faustine Kamuzora. Makabidhiano rasmi ya ofisi yatafanyika baadae. …