Ajali mbaya Iringa

Gari aina ya fuso lenye namba za usajili T115 ANZ likiwa limepinduka na mizigo kuzagaa baada ya kupata ajali mkoani Iringa jana. Katika ajali hiyo watu wawili walikufa na wengine 28 kujeruhiwa vibaya. (Picha na Francis Godwin, Iringa)

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu

Wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kufunguliwa kwa mkutano wao mkuu. Watatu kutoka kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani akifuatiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema na watano kutoka kulia ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju. (Picha …

Wafungwa wa kesi za EPA wakielekea gerezani

Washitakiwa katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Farijala Hussein na binamu yake Rajabu Maranda wakiwa katika ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi ndani ya gari wakati wakitoka Mahakamani kupelekwa gerezani baada ya kuhukumiwa miaka mitano jela.

Dk Mahanga asaidia vicoba Kimanga D’Salaam

MBUNGE wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga akikabidhi sh. 500,000 kwa umoja wa VICOBA katika Mtaa Tembomgwaza Kata ya Kimanga, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa umoja huo unaojumuisha vikundi 10 juzi.

Rais Kikwete ahani msiba wa Shekh Yahya Hussein

Rais Kikwete akipokewa na Hassan Yahya Hussein, Mtoto mkubwa wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein alipokwenda kuhani msiba wa mnajimu huyo maarufuf nyumbani kwa Marehemu Magomeni Mwembe chai Mei 22