Swala ya Idd jijini Dar es Salaam leo

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wakiswali swala ya Idd. Waislamu wote leo wameungana na Waislamu ulimwenguni kote kusherehekea Siku Kuu ya Idd baada ya kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. (Picha kwa hisani ya FullShangwe Blog).

Waziri Membe afanya mazungumza na Balozi wa Libya

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard K. Membe (Mb), akizungumza na Balozi wa Libya nchini, Profesa, Ahmed A. El Ash’hab baada ya balozi huyo kuitwa wizarani jana kufuatia ubalozi huo kubadilisha Bendera ya nchi bila kufuata taratibu. (Picha na Tagie Daisy Mwakawago wa Wizara ya Mambo ya Nje).

Ni foleni kila ‘sehemu’ jijini Dar es Salaam

Leo maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam yalikuwa na foleni kama yalivyokutwa na mpigapicha wa dev.kisakuzi.com. Pichani ni foleni barabara ya Morogoro eneo la Magomeni Mapipa. Hii ni foleni maene ya Mtaa wa Msimbazi Kariakoo. Pichani juu ni foleni ya magari eneo la Mnazi Mmoja. Foleni barabara ya Sekilango, Sinza. (Picha zote na Joachim Mushi)

Biashara ya nyanya Ilula

Wafanyabiashara wa zao la nyanya Ilula Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, wakinadi bidhaa zao kwa mmoja wa wateja hivi karibuni eneo hilo. (Picha na mpiga picha wetu)

Maonesho ya sita ya wajasiriamali wadogo Kanda ya Kusini

MAONESHO ya wajasiriamali wadogo na wakati katika sekta ya Viwanda yanayoratibiwa na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Kanda ya Kusini kufanyika mkoani Ruvuma mwaka 2011. Hayo yamesemwa hivi karibuni na Kaimu Meneja wa  SIDO, Mkoa wa Ruvuma Bw. Athur Ndedya. Bw. Ndedya akizungumza na wanahabari alisema “SIDO imekuwa utaratibu wa kuandaa maonesho ya wajasiriamali kikanda kila mwaka. Maonesho haya …