Wasomi 53 Wafyatua Matofali 45,000 Kujenga Mabweni…!

   Vijana wasomi 53 wa grupu la Whatsapp la WAZALENDO wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani, umbali wa kilomita 151 kutoka Dar es salaam, na kilomita 53 kutoka makao makuu ya Wilaya.  Leo wamekutwa wakifanya kazi hiyo nzito huku wakihamasika kwa nyimbo …

Kampuni ya TTCL, Huawei Wazinduwa Teknolojia ya 4.5G

    Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (katikati) akipiga makofi pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Tanzania, Bruth Zhang (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa …

Ujerumani Yachangia Milioni 12 Tamasha la Sauti za Busara

  Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, akibadilishana mkataba na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Balozi  Egon Kochanke, baada kumaliza kutiliana saini ya makubaliano ya kuchangia Tamasha hilo kwa mwaka 2017, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar. 

Jeshi la Polisi Latoa Tahadhali Wamiliki wa Magari Kinondoni

Na Dotto Mwaibale WAMILIKI wa magari wametakiwa kuchukua tahadhari ya kuzima na kufunga milango magari yao pale wanaposimama kwa dharura kupata mahitaji mbalimbali ili kuyanusuru kuibwa. Mwito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Suzan Kaganda wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu tukio la kuibwa kwa gari la Kapteni …