Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi, Clement Chagula na bintiye Olivia Chagula medali kwa niaba ya baba na babu yao Marehemu Dk. Wilbert Chagula, ambaye aikuwa ni mmoja wa mawaziri katika serikali ya awamu ya kwanza na mmoja wa watu maarufu waliotunukiwa nishani katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru. Chagula, ambaye ni mtoto wa marehemu, hakuweza kufika Dar es Salaam kupokea medali …
Rais Kikwete akiwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR)
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Desemba 15, 2011 ameungana na viongozi wenzake wa nchi wanachama wa Umoja wa Nchi za Maziwa wa International Conference on Great Lakes Region (ICGLR) kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka huu wa Umoja huo kwenye Hoteli ya Munyonyo Resort, nje kidogo ya mji mkuu wa Uganda wa Kampala. Miongoni mwa viongozi …
JK katika mazungumzo na Balozi wa Uturuki
Rais Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Uturuki aliyemaliza kufanya kazi nchini Dk. Sander Gurbuz aliyekwenda kumuaga leo Jumanne Desemba 13, 2011 Ikulu jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU)
Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Mtoto Tanzania wafanya uchaguzi
Kwa mujibu wa katiba ya Mtandao wa Malezi Makuzi na Maendleo ya Mtoto Tanzania, uchaguzi mkuu hufanyika kila baada ya miaka mitatu. Ni kidindi zaida ya miaka mitatu sasa tangu uchaguzi mkuu ufanyike na hii ni kutokana na ukosefu wa fedha ya kuitisha mkutano huu. Mkutano huu umekuwa ni wa lazima pia kutokana na mabadiliko ya katiba ambayo yamelenga kupunguza …