RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Desemba, 2016 ameungana na wananchi wenzake Wilayani Chato mkoani Geita kutoa pole kutokana na kifo cha Mzee Admirabilis Mbabe Manyama ambaye ni mzee maarufu wilayani hapa na Mzee James Lufunga Mchele ambaye ni jirani yake. Rais Magufuli pamoja na kuwapa pole wafiwa na …
Safari ya Mwisho ya Mpigapicha Mpoki Bukuku..!
Alice Mama wa Marehemu Mpoki Bukuku akisaidiwa kuweka shada la maua katika kaburi la mwanaye Mpoki Bukuku wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika Msalato nje kidogo ya mji wa Dodoma Marehemu Mpoki alifariki hivi karibuni jijini Dar es salaam kwa kugongwa na gari maeneo ya Mwenge. Watoto wa Marehemu Mpoki Bukuku Junior akiongozana na wadogo zake wakiweka shada la maua …
Mwadhama Kardinali Pengo Atoa Ujumbe Mkesha wa Krismasi…!
Kwaya ya Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Akbano ikitumbuiza katika ibada iliyofanyika katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam. Waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano wakiwa kwenye ibada ya mkesha wa krismasi. Vijana wa Kanisa la KKKT la Azania Front wakiigiza igizo la kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo. Kwaya ya Vijana ya KKKT usharika wa Azania Front ikitoa …
Kampuni ya TTCL yanogesha sherehe za Chrismass vituo vya watoto yatima Dar
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa pili kushoto) akimkabidhi mbuzi Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu …
Waziri Ummy Mwalimu Akipokea Nyumba 20 Kijiji cha Sese, Magu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), akikata utepe kuashiria upokeaji wa nyumba 20 mkoani Mwanza, zilizojengwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa. Nyumba 10 zimejengwa katika wilaya ya Ukerewe na 10 katika wilaya ya Magu. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), akikata utepe kuashiria upokeaji …