Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Chato mkoani Geita.
Kampuni ya TTCL yadhamini michuano ya vyuo Soka la Ufukweni
Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane Mwakalebela (wa tatu kushoto) akimkabidhi nahodha wa timu ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), Ally Rabi (wa tatu kulia) fedha shs 600,000/- pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa …
Wafanyakazi wa Jambo Leo Walivyo Ukaribisha Mwaka Mpya 2017…!
Wafanyakazi wa Gazeti la Jambo Leo linalochapishwa na Kampuni ya Quality Media Group Limited wakiwa na furaha wakati wa hafla ya kuukaribisha Mwaka Mpya 2017 kwenye Ukumbi wa Ground Zero, Kurasini Dar es Salaam juzi. Wakigongeana ikiwa ni ishara ya kutakiana heri ya Mwaka Mpya wa 2017. Wakicheza kwa furaha muziki uliokuwa ukiporomoshwa wakati wa hafla hiyo. …
Matukio Shamrashamra za Mkesha wa Mwaka 2017 Dar
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Akson, akipeperusha bendera ya Taifa wakati wa mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Dk. Akson alimwakilisha Rais Dk. John Magufuli kwenye mkesha huo ambaye alikuwa mgeni rasmi. Waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakiimba nyimbo za kumsifu mungu. Watoto …