Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa, amekishukuru kiwanda cha Saruji cha Rhino cha Tanga kwa msaada wake wa madawati 350 kwa shule ya Msingi ya Kange na mabenchi 10 kwa Zahanati iliyopo ndani ya kata hiyo. Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano, Mwalapwa alisema msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi darasani kukaa chini hivyo kutaka makampuni mengine kufuata nyayo za kiwanda hicho cha Rhino. …
Care International Tanzania Yawakutanisha Wadau wa Taasisi za Kifedha
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dkt Ashatu Kijaji akitoa hotuba yake wakati wa mkutano wa tatu wa kitaifa juu ya huduma za Kifedha kwa vikundi vya hisa, mjadala wa masuala ya kisera na kisheria katika uhusishwaji wa kifedha ulioandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Care International Tanzania, Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam. Mkurugenzi …
East African Ngwasuma Original Band Yawapagawisha Wakazi wa Kilimanjaro
Kiongozi wa band ya East African Ngwasuma Original Band Kingombe Blaise wa pili kulia akiwa anafanya mambo katika ukumbi wa Filomena Bar uliopo Boma Ngo’mbe mkoani Kilimanjaro wakati wa onyesho lao walilofanya mwishoni mwa wiki hii. Waimbaji na wanenguaji wa bendi ya East African Ngwasuma Original Band wakiwa wanawapagawisha wakazi wa Bomang’ombe na mitaa yake. Wanenguaji wa band …
TMA yatoa utabiri wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi leo ametoa utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017, huku utabiri huo ukionesha uwezekano mkubwa wa mvua za wastani katika maeneo mengi ya nchi. Dk. Kijazi ameongeza ya kuwa kutakuwa na mtawanyiko hafifu wa mvua na vipindi virefu vya …
Prof Waziri Mbarawa Uso kwa Uso na Bodi ya AfDB
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameiomba Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo Africa (AfDB), kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika mkakati wake wa kukuza uchumi kwa kuwekeza katika sekta ya miundombinu. Akizungumza na Wakurugenzi wa Bodi ya AfDB waliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Prof. Mbarawa ameishukuru benki hiyo kwa ushirikiano inaoipa Serikali ya …