Na Mwandishi Wetu, Mbinga UONGOZI wa Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) umekagua jengo ambalo umepanga kuweka mashine ya usindikaji wa zao la mhogo, wilayani Mbinga itakayotumiwa na kikundi cha MUVI kijiji cha Kilosa. Uongozi huo umefanya kazi hiyo hivi karibuni ulipotembelea kijiji hicho mkoani Ruvuma. Akizungumza katika ziara hiyo, Kaimu Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogovidogo (SIDO) mkoani Ruvuma, …
SIDO IRINGA KUTOA MAFUNZO YA USINDIKAJI
Na William Macha, Iringa SHIRIKA la Kuhudumia Viwanda nchini (SIDO) mkoni Iringa linatarajia kutoa mafunzo ya usindikaji bora bidhaa za chakula hivi karibuni. Akizungumza ofisini kwake meneja mkuu wa shirika hilo mkoani hapa, Gervase Kashebo amesema mafunzo hayo ya usindikaji wa mchuzi, nyanya mvinyo pamoja na bidhaa nyingine zitokanazo na matunda ya msimu yatawalenga wajasiriamali kutoka mkoani Iringa. Aidha ameongeza …
MUVI yaanza kutoa elimu kwa wakulima Njombe
Na William Macha, Njombe MRADI wa Muunganisho wa Wajasiriamali Vivijini (MUVI) kupitia kitengo chake cha habari umeingia Njombe na kufanikiwa kuzungumza na wajasiriamali wa zao la nyanya na alizeti kutoka mkoani humo. Katika hatua ya kwanza kitengo hicho cha habari kimefanya ziara kwenye vijiji vya Igongolwa, Lyamkena, Ikwete, Kiumba, Itipingi, Ibiki, Mahongole, Kifumbe, Uselule na Imalinyi. Wajasiriamali kutoka katika vijiji …
Wakulima watakiwa kuzingatia ushauri wa wataalam
Na Janeth Mushi, Arusha WAFUGAJI na wakulima nchini wametakiwa kufufanya shughuli zao kwa kufuata ushauri wanaopatiwa na wataalamu ili kuongeza uzalishaji pamoja na ubora wa bidhaa wanazozalisha. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mtaalamu wa Pembejeo za Kilimo na Dawa za Mifugo, kutoka kampuni ya Keenfeeder’s wasambazaji wa dawa za mifugo na kilimo, Anzamen Muro alipokuwa akizungumza na wakulima katika …
Zao la alizeti linaweza kukuza uchumi wa Tanga
Na Ngusekela David, Tanga MKUU wa Wilaya ya Handeni, Seif Mpembenwe amesema wakulima wa alizeti wataweza kuinua kipato chao mara dufu endapo watalima zao hilo la alizeti kwa kuzingatia kanuni za kilimo bora. Mpembenwa alisema hayo mjini hapa alipokuwa akifungua kikao cha pili cha jukwaa la wadau wa alizeti wilayani Handeni, ambalo limeundwa kwa lengo la kuwaunganisha wadau wa zao …