World Vision watumia bil 3.6 kuboresha shughuli za kijamii Manyara

Na Janeth Mushi, Simanjiro SHIRIKA la Misaada na Maendeleo ya Jamii ya World Vision Tanzania limetumia zaidi ya bilioni 3.6 kuboresha shughuli za kilimo, ufugaji na ujasiriamali kwa wakazi wa tarafa ya Moipo Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita. Taarifa hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Udhibiti na Ubora wa shirika hilo, Griffin …

Dk. Chami afungua maonesho ya wajasiriamali Mbinga

Na Dunstan Mhilu, Mbinga MAONESHO ya wajasiriamali wadogo na wakati Kanda ya Kusini yamefunguliwa rasimi na Waziri wa Viwanda na Biashhara Dk. Cyril Chami katika  viwanja vya CCM wilayani Mbinga.  Akizungumza na wajasiriamali hao pamoja na wakazi wa mbinga   aliwapongeza kwa ukarimu wao  wa kukarimu wageni nakuipongeza SIDO Mkoa wa Ruvuma kwa kufanikisha maonesho hayo.  Aidha amewataka wana mbinga na …

Njaa yawatisha Wanakijiji Matembo, Iringa

HALI ya chakula si nzuri katika Kijiji cha Matembo Jimbo la Ismani mkoani Iringa. Wanakijiji wa eneo hilo wanahitaji msaada wa chakula kutokana na hali mbaya ya upatikanaji wa chakula. Taarifa ambazo mtandao huu umezipata kaya nyingi zinakabiliwa na njaa, hali ambayo inatashia maisha ya wanakijiji hicho na baadhi ya maeneo mengine.

Biashara ya nyanya Ilula

Wafanyabiashara wa zao la nyanya Ilula Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, wakinadi bidhaa zao kwa mmoja wa wateja hivi karibuni eneo hilo. (Picha na mpiga picha wetu)

Kero ya maji ‘yawatibua’ nyongo wana-Ludewa

Na Mwandishi Wetu, Ludewa WANANCHI Ludewa Mjini, mkoani Njombe wamedai hawaoni umuhimu wa kuendelea kuwepo kwa Mamlaka ya Maji Ludewa Mjini (LUDWSSA) kwa sababu inaonekana kushindwa kutoa huduma kwa wananchi. Wakizungumza kwa nyakati na mtandao huu, wananchi hao walisema mamlaka hiyo imeshindwa kuwapatia maji ya uhakika, huku serikali ya wilaya hiyo nayo ikisuasua kuchukua hatua kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi. …