Ule Mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) unaendelea na shughuli zake (Picha zote na Dunstan Mhilu)
MUVI yatoa mafunzo ya Ujasiriamali na Uongozi wa Biashara
Na Ngusekela David, Tanga MRADI wa Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) umetoa mafunzo mbalimbali kwa wajasiriamali ili kuhakikisha inawajengea uwezo katika shughuli zao za kila siku na hatimaye kujikwamua kwenye lindi la umasikini. Mafunzo hayo yanayojulikana kama mafunzo ya ‘Ujasiriamali na Uongozi wa Biashara’ yamefanyika wilayani Handeni huku yakihusisha wakulima, mawakala wa pembejeo, wasindikaji pamoja na wadau anuai wa mnyororo …
Katibu Tawala Ruvuma azindua mashine ya kukamua alizeti kwa Wana-vijiji
Na Dunstan Mhilu, Ruvuma KATIBU Tawala Mkoa wa Ruvuma, Dk. Aselm Tarimo juzi amezindua mashine za kukamua mafuta ya alizeti katika Kijiji cha Mtyangimbole Wilaya ya Songea Vijijini. Katika uzinduzi huo aliwataka wananchi wa kijiji hicho na vijiji vya jirani kuhakikisha wanaitumia vizuri mashine hiyo ili iweze kuwanufaisha kihuduma. “Mashine imeletwa kazi ni kwenu, …leteni alizeti yenu ikamuliwe mpate mafuta …
MUVI yatoa mafunzo kwa waendesha Mashine za kukamua Mafuta ya Alizeti
Na Danstan Mhilu MUUNGANISHO wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) Mkoa wa Ruvuma umetoa mafunzo kwa waendesha mashine za kukamua mafuta ya alizeti mjini hapa. Mafunzo hayo yaliyofanyika Ofisi za Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), huku miongoni mwa wanavikundi waliopata mafunzo hayo wakiwa ni wana vikundi wapatao 20. Awali akifungua mafunzo hayo Kaimu Meneja wa SIDO, Ruvuma, Athur Ndedya aliwasihi wana …
Mafunzo ya Kilimo Biashara kuongeza tija kwa Wajasiriamali Tanga
Na Ngusekela David MRADI wa Muungano wa Wajasiriamali Vijijini (MUVI) unaendesha mafunzo ya kilimo kama biashara wilayani Muheza yanayotolewa na wakufunzi ambao ni maofisa ugani wa kata na vijiji katika Wilaya za Muheza, Korogwe na Handeni. Mafunzo hayo yanaratibiwa na mradi wa MUVI na yanahusisha kilimo cha alizeti na machungwa kwa Wilaya zote ambazo mradi wa MUVI unafanya kazi. Lengo …