Jamii za Kifugaji wasaidiwa ujenzi wa bweni
Na Mwandishi Wetu, Arusha MASHIRIKA mawili yasiyokuwa ya kiserikali (NGO’s) yanayotoa msaada na ushauri wa kisheria kwa jamii za kifugaji na wawindaji na kutetea haki zao, yametoa msaada wa zaidi ya sh. milioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Yaedachini wilayani Mbulu. Mashirika hayo ni PINGO’s Forum na UCRT ya mkoani Arusha, ambapo wametoa mabati …
Breaking Newzz: ‘Mchawi’ adondoka angani!
Na Mwandishi Wetu, Mkuranga TAARIFA ambazo zimetufikia ni kwamba mama mmoja (55) akiwa mtupu, yaani kama alivyozaliwa amedondoka kutoka angani alipokuwa akisafiri na ungo pamoja na mwanaye anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 9. Watu hao wanaoshukiwa kuwa washirikina wamedondoka usiku wa kuamkia leo eneo la Vikindu, Wilaya ya Mkuranga nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Shuhuda wa …
RC Tanga atembelea vitalu vya miche ya machungwa
Na Ngusekela David, Tanga MKUU wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa amefanya ziara fupi katika vitalu vya miche ya machungwa vinavyozalishwa na wakulima wa Kikundi cha Maduma kilichopo Kijiji cha Maduma Kata ya Mtindiro wilayani Muheza. Kiongozi huyo akiwa eneo la tukio amesifu juhudi zinazofanywa na wakulima wa Maduma na kuwashauri kuwa karibu na wataalamu wa kilimo ikiwa ni pamoja …
Makovu ya Nduli Amini hayata sahaulika- Askofu Kilaini
ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini, amesema makovu yaliyotokea katika vita vya Kagera vilivyoanzishwa na Nduli Idd Amini wa Uganda hayawezi kusahaulika kwa wakatoliki wa Kasambya na hata wana-Kagera wote. Kilaini ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akiwahubiri waumini wa Parokia Kasambya Kyaka na wageni anuai, kwenye Jubilee ya Miaka 75 ya kuanzishwa kwa Parokia hiyo iliyopo …
Wakulima wanogewa na mradi wa kilimo cha alizeti
Na Dunstan Mhilu, Ruvuma MUUNGANISHO wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) kutoka kikundi cha ’Moto Moto’ kilichopo katika Kijiji cha Amani Makoro, Kata ya Mkako wilayani Mbinga, umepanga kuongeza hekari nyingi kadiri ya uwezo katika msimu huu wa kilimo hususani katika zao la alizeti na mhogo. Taarifa hiyo ilitolewa hivi karibuni na Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho ambaye pia ni mwana kikundi, …