MUUNGANISHO wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) Mkoa wa Ruvuma hivi karibuni umetoa mafunzo kwa maofisa ugani (mabwana/mabibi shamba) wa Wilaya ya Mbinga. Hiyo ni moja ya jitihada za mradi huo kuhakikisha wakulima wa alizeti na mhogo katika mkoa huo wanapata elimu stahiki kuhusu ulimaji na utunzaji wa mazao hayo ambayo yana soko la uhakika mkoani Ruvuma. Akitoa mafunzo hayo Mkaguzi wa …
Wakulima walioathirika na mvua wapewa mbegu Mbeya
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbeya imetoa msaada kwa wananchi walioathirika na mvua zilizonyesha na kuharibu mazao katika kijiji cha Nsambya Kata ya Iwindi iliyopo katika halmashauri hiyo mkoani Mbeya. Msaada huo ulitolewa juzi na Mkuu wa wilaya hiyo, Evance Balama akiongozana na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Juliana Malange pamoja na mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini (CCM) Lackson Mwanjali na …
Wanafunzi walemavu wapimwe kiupekee – Walimu
Na Joachim Mushi, dev.kisakuzi.com-Arumeru BAADHI ya walimu wa wanafunzi wenye ulemavu anuai wilayani hapa wameitaka Serikali kuacha utaratibu wa kuwataini wanafunzi wenye ulemavu katika mitihani ya taifa kwa vigezo sawa hasa upande wa muda wa kufanya mitihani husika. Wamesema hali hiyo inawanyima baadhi ya wanafunzi wenyeulemavu kujipima kiusahihi kutokana na dosari zao na wanafunzi wa kawaida hivyo kujikuta wengi wakifanya …
Mradi wa Uwezeshaji Mifugo (Seed Stock) wa kifuta machozi cha mifugo
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amezindua Mradi Kabambe wa Serikali wa Uwezeshaji Mifugo (Seed Stock) wa kutoa kifuta machozi cha mifugo kwa maelfu ya wananchi katika wilaya tatu za Mkoa wa Arusha mifugo ambao walipoteza mifugo yao wakati wa ukame mkubwa ulioendelea kwa miaka mitatu mfululizo katika wilaya hizo. Rais Kikwete amezindua Mradi huo katika …