Wanafunzi walemavu Mafinga waipigia magoti Serikali

Na Joachim Mushi, dev.kisakuzi.com- Mafinga WANAFUNZI wenye ulemavu anuai katika Shule ya Msingi Makalala wameiomba Serikali na wadau wengine kuwasaidia kuwajengea mazingira bora ya kujifunzia kwa watoto wenye ulemavu ili waweze kupata elimu bora kama ilivyo kwa watoto wengine. Kauli hiyo imetolewa katika risala ya wanafunzi hao iliyosomwa jana Wilayani Mafinga kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika …

Wanakijiji wailalamikia Serikali Kuu

WANAKIJIJI wa kijiji cha Mkambarani Morogoro Vijijini, wameilalamikia Serikali Kuu na halmashauri ya Wilaya kwa kumuingiza mwekezaji kutoka Korea katika kijiji jirani cha Pangawe na kutumia rasilimali maji bure bila kuwashirikisha. Wananchi hao kutoka katika kijiji cha Mkambarani Kata ya Mkambarani wilaya ya Mororgoro vijiji na viongozi wao wa kata wameishutumu ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mkoa na Wizara ya …

Tunalaani mauaji ya wazee kwa imani za kishirikina

Tangu jana tumekuwa tunaadika habari maalum kuhusu mauaji ya vikongwe mkoani Geita. Habari hiyo imejikita katika tukio la hivi karibuni kabisa la Mei 10, mwaka huu ambalo wanawake wanne, Esther Konya (55), Lolensia Bangili (70), Kulwa Mashana (65) na Rosa Masebu (65) waliuawa kinyama mno na kundi la wananchi wakiwatuhumu kwa ushirikina ambao ulisababisha fisi kumla mtoto wa miaka mitano, …

Binti asimulia mamaye alivyouawa kinyama

Ni ukatili usioelezeka, ni kukosa hata chembe ya ubinadamu, hii ni simulizi ya kutisha ya binti aliyeshuhudia mama yake akicharangwa mapanga kutokana na imani za kishirikina. Hakuna uchungu zaidi duniani ambao mwanadamu huupata pale anapofiwa na mmoja wa wazazi wake awe mama ama baba. Uchungu huu huupata bila kujali kuwa kifo hicho kimesababishwa ama na maradhi au na umri kufikia …

‘Ashindwa kujiunga na Sekondari Handeni kwa kukosa ada’

Na Joachim Mushi, Handeni LICHA ya Serikali kuliarifu Bunge la Tanzania kuwa wanafunzi wote waliofaulu darasa la saba mwaka 2011 kutoka mikoa 12 tayari wamejiunga na kidato cha kwanza, imebainika bado kuna wanafunzi wameshindwa kujiunga na shule kutokana na kipato duni cha familia zao. Mwenjuma M. Magalu aliyechaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Komnyang’anyo wilayani Handeni ni miongoni mwa wanafunzi …

Sekondari za Kata Handeni zachochea mimba kwa wanafunzi

Na Joachim Mushi, Thehabari, Handeni WANANCHI wilayani Handeni wameilalamikia mazingira magumu kimiundombinu ya shule za sekondari za kata katika wilaya hilo na kudai ndiyo chanzo cha kuongezeka kwa mimba kwa wanafunzi na kukatisha masomo. Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti katika mahojiano ya baadhi ya wakazi wa Handeni na mwandishi wa habari hizi ndani ya uchunguzi uliofanywa hivi karibuni maeneo …