Je, Wajua Jinsi ya Kutunza Miti ya Michungwa..!

MITI ya michungwa inahitaji uangalizi wa hali ya juu, kitu ambacho wakulima wengi ama hawakijui ama hawakitilii maanani.miti hii hupandwa kwa mbegu za milimao ya kawaida (rough lemon) halafu inaungwa kwa kutumia vikonyo maalumu vya michungwa. Miti hii inahitaji ukaguzi wa mara kwa mara ili kupunguza matawi yanayokuwa bila mpangilio kwani matawi haya huzuia mti kupata hewa kwenye shina. Matawi …

CHAVITA Mkuranga Waomba Kusaidiwa Kielimu

Na Joachim Mushi, Mkuranga CHAMA cha Viziwi Wilaya ya Mkuranga (CHAVITA), kimeiomba Serikali na wadau wengine kuisaidia jamii hiyo ya walemavu iweze kupata fursa za elimu kama ilivyo kwa makundi mengine na hatimaye kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kijamii ambazo kwa sasa wanazikosa. Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mweka Hazina wa CHAVITA-Mkuranga, Bi. Subira Upuruje alipokuwa akimsomea …

Kangoye azungumzia maendeleo ya Benki ya Vijana

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya Tanzania Youth Development Agenda (TAYODA), imesema mchakato wake wa kuanzisha benki ya vijana kwa lengo la kuwakomboa na kupata mikopo kupitia benki hiyo, unaendelea na upo kwenye hatua nzuri. Mkurugenzi Mtendaji wa TAYODA, Jackson Kangoye, alisema hayo juzi wakati akizungumza na baadhi ya vikundi vya vijana wilayani Mpwapwa, Dodoma ambao wamekuwa wakiwezeshwa na taasisi hiyo …

Wanakijiji kuishtaki Serikali Umoja wa Mataifa

Augustine Mgendi, Buhemba WANANCHI wa vijiji vitatu wanaozungukwa na Mgodi wa Buhemba, Wilaya ya Butiama mkoani Mara wamekusudia kuishtaki Serikali ya Tanzania katika Taasisi za Umoja wa Mataifa zinazohusika na haki za binadamu ikiwa ni shinikizo la kulipwa fidia ya sh. bilioni 30. Mbali na kusudio hilo la kwenda Umoja wa Mataifa, wananchi hao wamepania kumuona Rais Jakaya Kikwete kumueleza …

Mama wa mwanafunzi aliyeshindwa kujiunga na sekondari Handeni afariki dunia

Na Joachim Mushi, wa dev.kisakuzi.com MAMA wa mwanafunzi Mwenjuma Magalu aliyechaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Komnyang’anyo wilayani Handeni na kushindwa kujiunga na shule hiyo kutokana na familia hiyo kutelekezwa na baba amefariki dunia. Mama huyo Hadija Magalu amefariki dunia juzi ikiwa ni muda mfupi baada ya kujifungulia nyumbani kwake hali iliyomfanya apoteze damu nyingi hatimaye kuzidiwa na kufariki dunia. …

Kituo cha afya chakatiwa umeme, wajawazito wajifungua na chemli

Na Joachim Mushi, dev.kisakuzi.com-Kishapu KITUO cha Afya kilichopo Kata ya Songwa, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kimekatiwa umeme kwa takribani miezi saba sasa kikidaiwa bili ya umeme na TANESCO ya jumla ya sh. 38,000 hali inayowabebesha mzigo wa gharama wananchi wanaofika kupata huduma kituoni hapo. Wagonjwa wanautibiwa usiku katika kituo hicho hasa wanawake wajawazito wanalazimika kugharamia mafuta ya taa kwenye …