Wanafunzi wala mlo mmoja

Na Mwandishi wa Daraja MOJA ya changamoto inayowakabili wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kipagalo na Shule ya Msingi Mahulu, zilizopo Makte Njombe ni kutopata chakula cha mchana wakiwa shuleni. Akizungumza na Shirika la Daraja, Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kipagalo, Ayoub Honelo anaeleza kusikitika kwake kwa hali hiyo huku akieleza; “inaumiza sana kuona mwanafunzi wa bweni anapata mlo mmoja …

Hatimaye mwalimu kuchekelea

    Na Mwandishi wa Shirika la Daraja HATIMAYE Shule ya Msingi Kibeto iliyopo Kijiji cha Madindo, Ludewa, Mkoa wa Njombe inatarajiwa kupata walimu baada ya kukaa tangu 2006 ikiwa na ikiwa na mwalimu mmoja. Shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 77, ina vyumba vitatu vya madarasa, ambapo wanafunzi wanasoma kwa kupokezana, huku pia ikikabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati …

Katavi Watakiwa Kulima Kilimo cha Kisasa

Na Anna NKinda – Maelezo, aliyekuwa Mpanda WAKAZI wa Katavi wametakiwa kulima kilimo cha kisasa na kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo ili waweze kuvuna mazao mengi zaidi ambayo yatawasaidia kupata chakula cha ziada ambacho kitawafaa wao na kuwasaidia mikoa ya jirani. Wito huo umetolewa jana na Mke Wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wananchi hao waliokusanyika katika …

Jerry Silaa Apongezwa Ujumbe Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM

Baadhi ya kinamama wa Gongo la Mboto ambao ni wananchama wa CCM wakiwasili kwenye Uwanja uliopo karibu na reli Gongo la Mboto katika mkutano wa hadhara wa kumpongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho …

Mke wa Rais Kikwete Awataka Wanalindi Kuendelea Kulima Mtama

Na Anna Nkinda – Maelezo , Lindi WANANCHI wa Mkoa wa Lindi wametakiwa kurudia kulima kwa wingi zao lao la chakula la mtama kwani zao hilo linastahimili hali ya ukame na hivyo kuweza kukabiliana na janga la njaa linaloukabili mkoa huo mara kwa mara. Wito huo umetolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa (NEC) …

Handeni, Kilindi Wazimia kwa Njaa

WAKATI wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha njaa ikisababisha baadhi ya wanaume kukimbia familia zao, Wilaya ya Handeni na Kilindi mkoani Tanga, baadhi ya wananchi wameanza kuzimia kwa kukosa chakula kwa muda mrefu huku wengine wakila mizizi. Habari zilizopatikana wilayani humo zinaeleza kuwa kuna watu 25 walioanguka na kupoteza fahamu kutokana na njaa inayolikabili eneo hilo. Miongoni mwa maeneo …