Room to Read Wajenga Madarasa 60 Wilayani Mvomero

Moja ya madarasa katika  Shule ya Msingi Dihinda iliyopo kata ya Mvomero ambalo limejengwa na Shirika la Room to Read. *Ni shirika pekee lenye mradi wa kuimarisha uwezo wa kusoma, kuandika na kuhesabu kwa watoto. *Tayari limefanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 60 katika shule za msingi 15 wilayani Mvomero. *Sasa laelekeza nguvu zake wilayani Bagamoyo na kukusudia kujenga madarasa …

Amuua Baba Yake kwa Ushirikina

JESHI la Polisi mkoani Rukwa linamsaka Richard Jecap (30) mkazi wa kitongoji cha Matai A kwa tuhuma za kumuua baba yake kwa kumpiga mpini kichwani akimtuhumu kuwa ni mshirikina. Tukio hilo lilitokea Aprili 18 saa 4.50 asubuhi wakati baba huyo akiwa amekaa nyumbani kwake akiota jua. Akizungumza na gazeti hili, mwenyekiti wa kijiji hicho, Emmanuel Mwakibinga alisema kuwa mtuhumiwa alifanya …

Ushahidi Kesi za Kubaka/Mimba ni Changamoto Handeni

Na Joachim Mushi, Handeni “KESI nyingi za tuhuma za kubaka na mimba kwa wanafunzi zinazotufikia zinashindwa kufikia hukumu maana mashahidi wanashindwa kuthibitisha pasipo shaka…nyingi zinaharibika sababu hawataki kusema ukweli, hivi karibuni nililazimika kuwaweka ndani wawili (mashahidi) kwa kuwa wanadanganya. Unakuta maelezo aliyotoa polisi ni mengine na akifika huku anageuka,” anasema Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi wa Wilaya ya Handeni, Patrick Maligana …

Mwanafunzi Kidato cha Pili Abebeshwa Mzigo Kulea Familia

Na Joachim Mushi, Handeni MWANAFUNZI wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Mwenjuma Magalu (16) amejikuta akibeba mzigo wa kulea familia baada ya familia hiyo kutelekezwa na babayake. Mwanafunzi huyo anayeishi katika Kijini cha Msasa amejikuta katika hali hiyo ngumu baada ya mama yake mzazi, Hadija Magalu kufariki dunia ambaye ndiye aliyekuwa akiihudumia familia hiyo baada ya mzazi mwenzake …

Mwenjuma Magalu: TAMWA Imerejesha Ndoto Zangu Kielimu

Na Joachim Mushi, Handeni “BAADA ya kumaliza darasa la saba nilichaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, lakini sikufanikiwa kuendelea na elimu hiyo kutokana na uwezo wa mzazi wangu mmoja (mama) ambaye alishindwa kumudu gharama zilizokuwa zikihitajika kwa wakati…,”ndivyo anavyoanza kusimulia Mwenjuma Magalu akizungumza Kijijini Msasa, Wilaya ya Handeni. Magalu anasema furaha zote alizokuwa nazo mwaka 2011 baada ya kuchaguliwa kujiunga …

Utafiti wa TAMWA Wamrudisha Mwanafunzi shuleni Handeni

Na dev.kisakuzi.com, Handeni UTAFITI wa kihabari uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 umefanikisha kumrudisha shuleni mwanafunzi wa sekondari aliyekuwa ametelekezwa yeye pamoja na familia yao. Mwenjuma Magalu ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo alitelekezwa na babayake yeye pamoja na mamayake mwaka jana, hivyo kushindwa kujiunga na …