WAKAZI wa Kijiji cha Twabagondozi wilayani Kibondo, Kigoma wamemuomba Waziri Mkuu Mizengo Pinda awasadie kuharakisha upatikanaji wa zaidi ya sh. milioni 660 ili waweze kukamilisha uchimbaji wa mfereji mkuu wa mita 2,500 katika mwaka 2013/2014. Wananchi hao wametoa ombi hilo Oktoba 3, 2013 wakati wakiwasilisha taarifa ya mradi wa ujenzi wa bwawa la umwagiliaji la Nyendara lililopo katika …
Waziri Pinda Kugawa Mizinga ya Nyuki 100 ya Kisasa Kibondo
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameahidi kutoa fedha za kununua mizinga kati ya 100 na 200 kwa ajili ya wanakijiji wa Biturana, wilayani Kibondo, mkoani Kigoma ambao wanajihusisha na uhifadhi wa misitu pamoja na ufugaji nyuki. Waziri Pinda ametoa ahadi hiyo Oktoba 3, 2013 wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kijiji hicho mara baada ya kukagua eneo la hifadhi …
Ugonjwa Usiojulikana Wamtesa Mwandishi wa Habari Tanga
Na Dotto Mwaibale, Tanga ZUBERI Mussa ambaye ni mpiga picha mkongwe katika vyombo mbalimbali vya habari nchini ambaye kwa sasa anafanyakazi kampuni ya New Habari ni mgonjwa anayehitaji msaada wa hali na mali. Kikubwa kinacho msumbua mwandishi huyu ni ugonjwa ambao haujafahamika, ambapo kwa mtu anayemfahamu ni rahisi kumgundua kuwa ana matatizo ya kiafya kwani katika kila sentesi yake ya …
Ni Ukatili wa Kutisha, Mume Amnyonga Mkewe Hadi Kufa
MWANAMUME mmoja amemnyonga hadi kufa mke wake na yeye akauawa na wananchi wenye hasira, katika Wilaya ya Bunda mkoani Mara. Tukio hilo lililothibitishwa na polisi wilayani hapa, lilitokea usiku wa kuamkia juzi katika Kijiji cha Kisangwa Kata ya Mcharo, kwenye sherehe ya ufunguzi wa nyumba ya ndugu yao. Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mcharo, Waziri Kingi, alimtaja mwanamke aliyeuawa kwa …
Maji Yawatesa Akinamama na Wanafunzi Kishapu
Na Joachim Mushi, Kishapu WASWAHILI wanasema ‘maji ni uhai’ na maisha bila maji ni kadhia. Kimsingi mwanadamu anahitaji maji safi na salama katika kuendesha maisha yake ya kila siku. Na kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama eneo fulani huchangia kiwango fulani cha ugumu wa maisha kwenye familia. Hali hii ndiyo inayowakumba wakazi wa baadhi ya vijiji vya Kata …
Uzazi Pasipo Mipango Unavyowatesa Wanawake Kishapu
Na Joachim Mushi, Kishapu WASUKUMA ni moja ya makabila nchini Tanzania ambayo awali yalishikilia desturi ya familia kuwa na idadi kubwa ya watoto. Familia moja yaani baba na mama waliendelea kuzaa kadri walivyo jaaliwa kupata watoto bila kujali ukubwa wa familia. Mume pia hakuwa na kizuizi katika familia cha kuongeza mke mwingine endapo atakuwa na ardhi (mashamba) na mifugo (hasa …