JK Ahaidi Kuongeza Kasi ya Usambazaji Umeme na Maji Vijijini

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Serikali yake itaongeza kwa kiasi kikubwa kasi ya kusambaza huduma za umeme na maji katika vijiji nchini kwa nia ya kuboresha maisha ya wananchi. Rais Kikwete amewaambia mamia kwa mamia ya wananchi wakati alipozindua miradi ya maendeleo, Novemba 27, 2013, katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi …

Baba Mzazi Ambaka Mtoto Wake wa Kike wa Miaka Sita

Na Yohane Gervas, Rombo POLISI wilayani Rombo inamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Martini Shayo (71) mkazi wa Kijiji cha Mengeni Chini Wilaya ya Rombo kwa kosa la kumbaka mwanaye wa kike mwenye umri wa miaka sita. Mkuu wa Polisi (OCD) wa Wilaya ya Rombo, Ralph Meela akizungumza na mtandao huu alisema kuwa tukio hilo limetokea Novemba 18, 2013 …

Kero ya Maji Rombo: Wananchi Wageuka Mafundi Wajiunganishia Maji

Na Yohane Gervas, Rombo TATIZO la ukosefu wa maji katika Kijiji cha Alen chini limechukua sura mpya baada ya wananchi kuamua kufukua mabomba ya maji na kujiunganishia maji wenyewe. Wakizungumza na Mtandao huu wananchi hao walisema wameamua kufikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa mafundi wa kampuni ya maji ya Kiliwater waliyafunga maji hayo yasielekee ukanda wa chini makusudi. Mmoja …

Mafunzo Kuhusu Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake Chalinze

Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima (kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba (kulia) kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi …

Ajinyonga kwa Mtandio Chumbani Mwake

Yohane Gervas, Rombo MWANAMKE mmoja aliyetambulika kwa jina la Maria Evansi (42) mkazi wa Kijiji cha Kaswira, Nanjara Kibaoni, Tarafa ya Tarakea wilayani Rombo amekutwa akiwa amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia mtandio chumbani kwake. Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Rombo, OCD, Ralph Meela, amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa nne asubuhi. Shuhuda wa tukio hilo ambaye …

Askari wa Operesheni Saka Majangili Walalamikiwa Kuchoma Nyumba za Wanakijiji Kabage, Mpanda

Hapa ndipo wanapoishi watu hawa baada ya nyumba zao kuchomwa moto. Watoto wakiwa michezoni huku wasijue watalala wapi ukifika usiku Hizi ndizo nyumba zao, wanalala chini ya miti baada ya nyumba zao kuchomwa moto. Wakazi wa kijiji cha kabage wakihama kijiji hicho baada ya nyumba zao kuchomwa na askari waliokuwa wanafanya oparesheni ya kuwasaka majangili nyumba hizo zilichomwa wiki iliyopita kijijini hapo …