Mahakama Nkasi Yalalamikiwa Kuvunja Ndoa Yenye Mgogoro Bila Kugawanya mali

Na Joachim Mushi, Nkasi MAHAKAMA ya Mwanzo Namanyere wilayani Nkasi imelalamikiwa kwa kitendo cha kuvunja ndoa iliyokuwa na mgogoro kwa wanandoa bila kugawanya mali iliyochumwa kipindi cha wanandoa wakiishi kama mke na mume. Bi. Maria Tarafa (25) mkazi wa Kijiji cha Isale ambaye ni mmoja wa wanandoa hao ametoa malalamiko hayo hivi mjini hapa alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari …

Vijana Watakiwa Kujiunga Kukabiliana na Umaskini

Yohane Gervas, Rombo VIJANA wilayani Rombo wametakiwa kufanya kazi kwa bidii sambamba na kujiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali ili waweze kukabiliana na umasikini unaowakabili. Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa asasi ya Kiraia ya umoja wa vijana wa wilaya ya Rombo (UVIWARO), Neema Mremi wakati alipokuwa akizungumza na vijana wa wilaya hiyo katika mkutano Mkuu wa mwaka wa asasi hiyo. …

Mwalimu Shule ya Msingi Amtia Mimba Mwanafunzi Wake na Wasekondari

Na Joachim Mushi, Namanyere-Nkasi MWALIMU mmoja wa Shule ya Msingi Sintali (jina tunalo) anatuhumiwa kwa kuwatia mimba wanafunzi wawili mmoja akiwa wa shule anayofundisha yeye na mwingine wa Shule ya Sekondari Sintali hali iliowafanya wanafunzi hao kukatisha masomo. Tukio hilo limetokea Katika Kijiji cha Sintali, Wilaya ya Nkasi na baada ya taarifa kuenea kijijini hapo mwalimu huyo alitoroka kituo chake …

Aowa Wanafunzi Mtu na Dada Yake

Na Joachim Mushi, Nkasi JESHI la Polisi Wilaya ya Nkasi kupitia dawati la Jinsia na Watoto, linamshikilia Pius Jacob Mkazi wa Kijiji cha Chala kwa kosa la kuoa mtu na dada yake, ambapo mdogo mtu alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kabwe wilayani Nkasi. Jacob alikamatwa na Polisi wa Dawati la Jinsia na watoto Kituo …

Polisi Wapeleka Kikosi Maalum Kuwasaka Waliovamia Kituo Malinyi

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi Tanzania, limepeleka timu maalumu ya askari kutoka makao makuu kwenda wilayani Ulanga, Mkoa wa Morogoro katika Operesheni ya kuwasaka na kuwakamata baadhi ya wananchi waliovamia kituo cha Polisi na kukichoma moto pamoja na kuharibu mali zakituo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SSP – Advera Senso, Mkuu wa Jeshi …

Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Ataka Walevi Kudhibitiwa Rombo

Yohane Gervas, Rombo MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Rombo kuhakikisha anawaagiza viongozi wote wa vijiji vya wilaya ya Rombo kuweka mikakati na sheria ndogo ndogo kwa kila kijiji za kukabiliana na tabia ambazo hazikubaliki katika jamii ikiwemo vitendo vya ulevi. Gama aliyasema hayo hivi karibuni wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mokala …