Yohane Gervas, Rombo WALIMU wawili wa Shule ya Sekondari Ubaa iliyopo katika tarafa ya Mkuu Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wanatuhumiwa kumshambulia na kumjeruhi vibaya kwa fimbo mwanafunzi wa kidato cha nne, Loveness Minja kwa kile kinachodaiwa kuwa alikataa kulipa shilingi 2,500 kwa ajili ya sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wa kidato cha kwanza (welcome form one). Mkuu wa shule hiyo, …
Ahukumiwa Miaka 30 kwa Kumbaka Mwanafunzi Std II
Yohane Gervas, Rombo MAHAKAMA ya Wilaya ya Rombo imemuhukumu Joseph Didas (39) mkazi wa Kijiji cha Ubaa Tarafa ya Mkuu Wilaya ya Rombo kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili. Awali mwendesha mashtaka Mkaguzi wa Polisi, Berndad Machibya amedai mahakani hapo kuwa Mshtakiwa mnamo mwezi Julai, 2013 kwa siku …
Zuio la Unywaji Pombe Rombo Lagonga Ukuta
Yohane Gervas, Rombo LICHA ya juhudi mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Serikali katika Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro za kuzuia ulevi muda wa kazi pamoja na usambazaji na uuzaji wa pombe haramu ya gongo bado imeonekana suala hilo kushika kasi katika maeneo mbalimbali katika wilaya hiyo. Serikali wilayani humo ilipiga marufuku mtu kunywa au kuuza pombe muda wa kazi, yaa ni …
Mwanamke na Changamoto za Maisha Vijijini
MWANAMKE maeneo anuai amekuwa akikumbana na changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku, lakini kwa kundi la wanawake vijijini changamoto hizi zimekuwa ni maradufu ukilinganisha na zile za wanawake wanaoishi mjini na wenye fursha mbalimbali. Zifuatazo ni baadhi ya changamoto hizi ambazo hukumbana nazo wanawake vijijini kwa makundi anuai katika matukio ya picha zilizopigwa na mwandishi wa dev.kisakuzi.com maeneo husika.
Maria: Mume Aliyenikatisha Darasa la Sita, Kanitelekeza na Watoto Wanne
Na Joachim Mushi, Aliyerejea Nkasi MATUKIO ya utelekezaji wa mke na watoto nchini Tanzania bado ni changamoto kubwa katika jamii. Licha ya matukio haya kutofautiana kutoka eneo moja hadi lingine bado yanachochewa na kulegalega kwa sheria za nchi ikiwemo sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kwa baadhi ya vipengele. Waathirika wakubwa wa matukio haya ni mama pamoja na watoto ambao …
Maria: Mume Wangu Aliiongopea Mahakama Ikavunja Ndoa Yetu
Nkasi, Rukwa NOVEMBA 18, 2013 Mahakama ya mwanzo, Namanyere, Wilaya ya Nkasi iliamua kuvunja ndoa ya Ndebile Kazuri na Bi. Maria Tarafa wote wakazi wa Kijiji cha Isale Mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa. Ndoa hiyo ambayo hadi mahakama inaivunja ilikuwa na watoto wanne, yaani watoto wawili wakiwa na miaka 9 na 7 huku wengine wawili wakiwa …