Serikali Yaombwa Kudhibiti Utengenezaji Pombe Kienyeji

Na Mwandishi Wetu, Rombo SERIKALI imeombwa kudhibiti utengenezaji holela wa pombe za kienyeji katika Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ambao umekuwa hauzingatii afya ya mtumiaji. Baadhi ya viongozi wilayani hapa wameshauri pombe hizo sasa kuangaliwa ili zitengenezwe kwa kuzingatia viwango vinavyo faa kwa afya ya watumiaji na kuiwezesha serikali kupata mapato. Ombi hilo limetolewa na madiwani wa halmashauri hiyo walipokuwa …

Watoto Nkasi Waajiriwa kwa Ujira wa Ndama kwa Mwaka

Na Joachim Mushi, Nkasi BAADHI ya watoto Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa hasa maeneo ya vijijini wamekuwa wakiajiriwa na familia za kifugaji kwa ujira wa ndama mmoja kwa mwaka mmoja. Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi watoto hao wengi wao ni wa kabila la Wafipa na wamekuwa wakitumikishwa kazi ya kuchunga ng’ombe za wafugaji wa kabila la Kisukuma. …

Madiwani Wawabana Watendaji wa Vijiji na Kata Rombo

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo limetoa utaratibu mpya wa kuwabana watendaji wa vijiji na kata wasio toa taarifa za mapato na matumizi kwa wanakijiji wao ambapo kwa sasa watakuwa wakiwasilisha taarifa hizo katika kikao cha awali cha baraza la madiwani. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango, Protasi Lyakurwa ambaye pia ni …

Mipango ya Wanajamii ni Muhimu Katika Kusimamia Wanyamapori – UNDP

KIONGOZI wa UNDP aliyeko ziarani nchini Tanzania, Helen Clark, amesema usimamizi wa maliasili unaoshirikisha jamii ni ufumbuzi wa muda mrefu na wenye ufanisi zaidi kwa ujangili wa tembo na biashara haramu ya wanyamapori. Akizungumza na watu kutoka vijiji 21 karibu na Hifadhi ya Taifa Ruaha alijifunza uzoefu wao na changamoto za usimamizi katika uhifadhi wa wanyamapori. ‘Ni wazi,’ alisema, ‘kila …

Walimu Wapya Wilaya ya Handeni Waonja Joto ya Jiwe

Na Joachim Mushi WAAJIRIWA wapya wa fani ya ualimu wa shule za msingi katika Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga wameanza kazi kwa kuonja machungu ya madeni baada ya kutopewa stahili zao zote kabla ya kuanza kazi na kusambazwa kwenye vituo vyao vya kazi kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo. Wakizungumza na dev.kisakuzi.com kwa masharti ya kutotaja majina yao kwa …

Wananchi waomba Kituo cha Afya Simambwe Kufanya Kazi Saa 24

Na Joachim Mushi, Tembela, Mbeya WANANCHI wa Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini wameiomba Serikali kusaidia kukiwezesha Kituo cha Afya Simambwe ili kifanye kazi saa 24 ili kuwasaidia muda wote wananchi wanaohudumiwa na kituo hicho hasa wajawazito. Kauli za ombi hilo zimetolewa hivi karibuni kwa nyakati tofauti na wananchi hao walipokuwa wakizungumza na mwandishi wa habari hizi katika vijiji …